THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

JIANDIKISHE SASA KUSHIRIKI MAONESHO YA SITA YA VITO JIJINI ARUSHAORODHA YA MAJINA YA WATUMISHI WA UMMA WANAODAIWA KUWA NA VYETI FEKI

NSSF YASAIDIA UJENZI WA ZAHANATA KATIKA KIJIJI CHA MATAMA MKOANI RUVUMA


SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa kituo cha Afya katika Kata ya Muhukuru, Kijiji cha Matama, Mkoani Ruvuma.

Vifaa hivyo, ni mifuko 800 ya saruji na nondo 400 zitakazosaidia kufanikiwa ujenzi wa kama njia yakuleta maendeleo katika jamii.Katika kufanikisha ujenzi huo, NSSF imetoa mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo zipatazo 400.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji, alisema NSSF ni shirika kubwa la hifadhi ya jamii lenye ofisi katika kila mkoa wa Tanzania na wilaya zake.

Mpango wa ujenzi wa zahanati hiyo umetokana na ombi la Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa NSSF kuona jinsi ya kusaidia jamii inayoshi katika Kata ya Muhukuru ambao walikuwa wanatumia kilometa 62 kufika katika zahanati ya Muhukuru.

Msaada huo wa NSSF, unalenga kufanikisha mpango huo wa kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za afya, hivyo kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukabidhi vifaa vya ujenzi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.

Naye Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu alisema msaada huo umekuja kwa wakati muafaka kwani baada ya kukamilika, utapunguza kero wanayopata wakazi wa kijiji cha Matama.

Aidha, diwani huyo aliongeza kuwa ujenzi huo utasimamiwa kwa ukaribu kuhakikisha hakuna atakayehujumu ujenzi wa kituo hicho na kutoa wito kwa wengine kuiga mfano huo wa NSSF.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Oraleti Komando, akipokea sehemu ya msaada wa mifuko 800 ya saruji na nondo 400 kutoka kwa Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji. Hafla hiyo ilifanyika mkoani Ruvuma mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Oraleti Komando, akimkabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na NSSF kwa Diwani wa Kata ya Muhukuru, Manfred Mzuyu. Kulia ni Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji.

Meneja wa NSSF Mkoa wa Ruvuma, Mariam Muhaji (wa tatu kulia), Ofisa Mwandamizi wa Masoko na Uhusiano, Amina Mmbaga (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na maofisa wengini wa NSSF baada ya kukabidhi mifuko 800 ya saruji pamoja na nondo 400 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati katika Kijiji cha Matama, Songea.
Wakzi wa Kijiji cha Matama Kata ya Mahukuru wakiwa katika hafla hiyo.
Sehemu ya msaada wa mifuko ya saruji iliyotolewa na NSSF kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Matama, Songea mkoani Ruvuma.


TAARIFA POTOFU ZINAZOMHUSISHA BALOZI WA TANZANIA NCHINI UINGEREZA DKT ASHA-ROSE MIGIRO

Ubalozi wa Tanzania London umepokea Habari inayozagaa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa instagram ikiwa na nukuu ifuatayo:

''Binafsi bado sijaona umuhimu na mafanikio ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zaidi ya vingozi kujikusanyia mali na utajiri mkubwa sambamba na kung'an'gania madaraka kwa nguvu. Mfano uchaguzi uliofanyika mwaka 2015 kwa yaliyotokea Zanzibar ni miongoni mwa Athari mbaya kabisa zinazotokona na Muungano,nadhani kila Mtanzania aliyaona"

Ukurasa huo wenyewe jina la UKUTA inaihusisha nukuu hiyo na jina la Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt Asha Rose Migiro. 

Ubalozi wa Tanzania London unapenda kutumia fursa hii, kuwajulisha Watanzania Waishio Uingereza na Watanzania kwa ujumla kuwa Balozi Migiro ahusiki na nukuu hiyo kama inavyosambazwa.Hivyo ni wazi kuwa wanayoisambaza wana malengo ya kulichafua jina la Balozi Migiro kwa sababu wanazozijua wao. 

Ubalozi wa Tanzania London unaendelea kutoa wito kwa Watanzania Waishio Uingereza kutumia muda wao na mitandao ya kijamii kutoa mawazo chanya yatakayo imarisha Muungano wa Taifa letu na mustakabali wa maendeleo ya Nchi yetu na Watanzania wa pande zote za Muungano. 

Ubalozi wa Tanzania London 
29 Aprili 2017.RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ASHIRIKI IBADA YA JUMAPIL MJINI MOSHI

Rais Dkt John Pombe Magufuli amejiunga na waumini kwenye ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kaskazini Usharika wa Moshi Mjini asubuhi hii. Rais Magufuli yuko mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu


MBUNGE WA BUKOMBE AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA VYAMA NA KUWA WAMOJA

Wananchi wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo zinaweza kusababisha kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo la hilo Dotto Biteko wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua changamoto walizo nazo.

Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.

"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe wazazi mshirikiane na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .

Hata hivyo ameongezea kuwa kwa vijana wameanza kutenga asilimia kumi ya mapato na tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.

Pia amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na kuwaambia kama wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao waliwaomba kura wakati wa kampeni.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akiwa kwenye Mkutano wa kutatua na kusikiliza Kero za wananchi kijiji cha Bwenda Kata ya Kantente.
Meza Kuuu hakiwepo Mbunge wa Jimbo la Bukombe pamoja na viongozi wa Kijiji cha Bwenda na wa kata ya Kantente. 
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambayo ilikuwa imeombwa na vijana kwaajili ya kujiandaa na Kombe la Dotto Cup 
Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuf Mohamedi akielezea wananchi juu ya serikali ambavyo imejipanga kutatua Kero za wananchi juu ya Elimu pamoja na Huduma ya Afya.JUMUIYA YA WATANZANIA WANAOSOMA BEIJING WAADHIMISHA MIAKA 53 YA MUUNGANO


Mwenyekiti wa Jumuiya ya watanzania wanaosoma Beijing Nchini Husein Mtoro ( katikati) aliyemwakilisha Balozi,aliambatana na Viongozi wote Wakuu akiwemo Makam Mwenyekiti Khamis Ngwali,Katibu Mkuu Ndugu Remidius Emmanuel,Naibu Katibu Mkuu Ndugu Alinanuswe Mwakiluma na Mweka Hazina Ndugu Kulwa Gamba.
 
Pamoja nao,Viongozi waasisi wa Umoja huo Ndugu Suleiman Serera na Irenius Kagashe nao walishiriki sambamba na Viongozi wastaafu wengine akiwemo Makam Mwenyekiti Mstaafu Ndugu Kassim Jape,Katibu Mkuu Mstaafu Angelina Makoye,Mtunza Hazina Mstaafu Lusekelo Gwassa katika maadhimisho ya muungano yaliyofanyika mapema wiki hii kwa kushriki maonesho ya utalii na utamaduni.
Baadhi ya watanzania wanaosoma katika chuo cha Beijing nchini China wakiwa katika maonesho ya utamaduni na utalii kama moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii.
Wadau wakipozi kwa picha
Maonesho ya utalii na utamaduni yakiendelea Jijini Beijing

Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania wanaosoma nchini China,wameadhimisha kumbukumbu ya Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kushiriki MAONYESHO YA KIMATAIFA YA UTALII NA UTAMADUNI katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Biashara na Uchumi jijini Beijing.
 

Akizungumza kwa niaba ya Balozi wa Tanzania nchini China Balozi MBELWA KAIRUKI,Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo,ndugu HUSSEIN MTORO aliwaasa Watanzania hao kudumisha Amani,Mshikamano na kushiriki katika ajenda muhimu za Taifa ikiwemo,kushiriki katika kukuza soko la Utalii kwa kutangaza Vivutio vya asili vya nchi yetu,kuhamasisha Watalii wengi wa kimataifa kutembelea vivutio mbali mbali vilivyopo Tanzania.Pia Mwenyekiti alifikisha salam za Balozi Mbelwa za kuwatakia kila la heri Wanafunzi wote walio katika hatua mbalimbali za kukamilisha Tafiti zao kwa ajili ya kukamilisha masomo yao.


MKUU WA MKOA WA PWANI MHANDISI NDIKIRO AISHUKURU TANESCO KWA MSAADA WA VIFAA VYA USAFI.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.

Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.

"Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi." Alisema.

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO kama mtoa huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi." Alisema.

Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. "Tumeungana nanyi leo Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali yawe safi." alsiema

Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro, aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya kituo hicho cha afya.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiri, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meenja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha Aprili 29, 2017.
Mhandisi Ndikiro, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake
Bi leila Muhaji, (katikati), akitoa hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga.


MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRIL 30,2017


RAIS DKT MAGUFULI APATA MAPOKEZI MAKUBWA MKOANI KILIMANJARO LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017 
Wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha Rais Magufuli wakimshangilia  wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi Karanga Wilaya ya Moshi mjini waliofunga barabara kumsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro
 Mbunge Mstaafu na Mwalimu maarufu nchini Mwalimu Kham akimtyambulisha Rais Magufuli kwa mamia ya wanafunzi waliojitokeza kumlaki
 Sehemu ya maelfu ya Wananchi wakimshangilia Rais Magufuli wakati akiongea nao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiongea na wananchi wa Bomang'ombe Wilaya ya Hai waliomsimamisha wakati akitokea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro alipowsili tayari kwa kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu mkoani humo Kilimanjaro Jumamosi Aprili 29, 2017.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA


RAIS DKT. MAGUFULI AAGIZA UWANJA WA MICHEZO WA KISASA DODOMA UJENGWE KARIBU NA UWANJA WA NANENANE


RAIS DKT. MAGUFULI AAGIZA HATI ZA ARDHI DODOMA ZIWE NA UMILIKI WA MIAKA 99


RAIS DKT. MAGUFULI ARIDHIA OMBI LA UDOM KUSAMEHEWA KODI YA ARDHI


Daladala, bajaji zisizokuwa na 'dustbin' kutozwa faini - DC wa Ilala Mhe. Sophia Mjema

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kufanya kwa vitendo kampeni ya usafi ya kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Sophia  Mjema akiwa kaongozana na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mhe. Edward Mpogolo alitembelea kituo cha daladala cha stesheni na kukuta magari mengi ya abiria hayana vikapu vya taka, ambapo wameyatoza takribani magari saba  kiasi cha shilingi 50,000 kwa kila moja katika eneo hilo.
Huku kwa upande wa madereva wa bajaji wanaopaki eneo la Soko la Samaki Feri wamepewa onyo na kuombwa kufanya hivyo mara moja kabla hawajachuliwa hatua na mamlaka husika ya Halmashauri hiyo ya Ilala.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wafanyabishara wadogo wanaopanga bidhaa zao kandokando ya barabara iliyopo jirani na soko la samaki la Feri kujiandikisha kwa afisa mtendaji na kuondoka eneo hilo mara moja, huku akisema Halmashauri hiyo itawapangia maeneo ya biashara ndani ya soko hilo.


SIMBA YATANGULIA FAINALI YA FA

Mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ (kushoto), akishangilia na beki wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ baada ya kufunga bao pekee katika mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Azam FC uliofanyika leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Himid Mao akichuana na Mohamed Ibrahim.
Mashabiki wakishuhudia mchezo huo huku wakinyeshewa na mvua.
Kocha wa Simba Joseph Omog akipeana mkono na kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche.
Waamuzi wakitoka chini ya ulinzi baada ya mchezo kumalizika.Ngoma Africa band watua kwa Wayahudi kutumbuiza sherehe za uhuru wa israel

Habari nyeti zimevuja sasa hivi kuwa Ngoma Africa band aka FFU UGHAIBUNI  bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya yenye makao kule nchini Ujerumani inatua nchini Israel kutumbuiza katika onyesho maalum la siku ya uhuru wa nchi hiyo ijulikanayo kama  Yom Haatzmaut siku ya tarehe 1 mpaka 2 Mei 2017 mjini Tel Aviv.
Mmoja ya wanaitifaki wa maonyesho hayo Bi.Shimone amesema bendi hiyo ndio ya kwanza ya Kiafrika kupata mwaliko wa kutumbuiza katika maonyesho hayo lakini hakutaka kuelezea zaidi.
Habari zaidi za uhakika zimevuja kuwa bendi hiyo imesafiri kimya kimya kutoka Ujerumani kuelekeahuko Uyahudini kwa ajili ya onyesho  hilo. Kiongozi wa bendi hiyo Kamanda Ras Ebrahim Makunja amethibitisha mwaliko huo wa kihistoria na kuiambia Globu ya Jamii kwamba wao hivi sasa wako Tel Aviv wakingoja kumwaga lazi.
 Kiongozi wa The Ngoma Africa Band wana FFU UGHAIBUNI akiongoza gwaride kujiandaa na libeneke la Israel
 Nyomi ya The Ngoma Africa Band wana FFU UGHAIBUNI katika moja ya maonesho yao
Kikosi kazi cha The Ngoma Africa Band wana FFU UGHAIBUNI


JARIDA LA WIZARA YA ARDHI , NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

TOLEO Na. 8 LA JARIDA LA WIZARA YA ARDHI , NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa jarida lake la mwaka (Toleo Na. 8). Jarida hili haliuzwi. Kuna nakala chache ambazo zinapatikana Wizarani katika Kitengo cha huduma kwa mteja. Aidha, kutakuwa na nakala nyingine chache ambazo zitasambazwa katika maeneo mbalimbali kama; Wizarani na katika Ofisi za Halmashauri nchini.
Jarida hili litapatikana pia hivi karibuni kwenye tovuti ya Wizara (www.ardhi.go.tz).

Mwananchi pata nakala yako upate kuhabarika kuhusu shughuli na matukio mbalimbali ya Wizara.

Na. Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 


Salaam Salaam introducing New song from Ujamaa Hiphop Darasa


HARAMBEE YA KUCHANGIA VIJANA WETU WA SERENGETI BOYS

video


DHANA YA ULIPAJI WA KODI YA PANGO LA ARDHI


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa tahadhari kwa wadaiwa wa kodi ya pango la Ardhi kwa kutoa elimu ya kuhusu dhana ya Kodi hiyo.

Hivi karibuni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa mafunzo mafupi kwa waandishi wa habari kwa nia ya kuhamasisha ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi na kubainisha utofauti wake kati ya kodi hiyo na Kodi ya Majengo ambayo hukusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA).

Akizungumza na waandishi wa habari; Mkuu wa Kitengo cha Kodi; Dennis Masami alisema; Dhana ya ulipaji wa kodi ya pango la Ardhi inatokana na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 katika fungu la 3 kifungu kidogo cha 1 (a) kinachosema: ‘Itambulike kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali ya Umma iliyowekwa chini ya Mheshimiwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya wananchi’’

Aliendelea kusema kuwa; Mfumo huu wa umiliki wa ardhi unatambulika kama lease hold na sio free hold, ambapo aina hii ya umiliki ni upangaji katika ardhi, ambao mpangaji anawajibika kufuata masharti ya upangishaji, mojawapo ya masharti hayo ni kulipa pango la kipande cha ardhi. Ambayo Mmiliki ni Rais kwa niaba ya umma na mpangaji ni Mwananchi.

Naye Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Mhe. William Lukuvi ametoa tahadhari kwa wasiolipa Kodi ya Pango la Ardhi akisema; “Wale wote ambao hawajalipa Kodi ya Pango la Ardhi, wote wanao miliki viwanja na mashamba yaliyopimwa, wahusike kulipa kabla ya mwisho wa mwezi wa sita (6). Ifikapo tarehe 30/06 hatua zifuatazo zitachukuliwa dhidi yao; Watashitakiwa Mahakamani, Mali zao zikamatwe na majengo yapigwe mnada kupitia madalali na Miliki zao zifutwe.

Alisema hatua hizo zote zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria, na kutoa tahadhari kuwa kila mmoja achukue hatua ya kulipa kwa hiari kwa Maendeleo ya Taifa.

Na kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  
Mkuu wa kitengo cha Kodi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dennis Masami akitoa mada kuhusu Maana na Umuhimu wa ulipaji Kodi ya pango la Ardhi kwa Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Wizara hiyo.


Taarifa kuhusu uzinduzi wa bodi ya kima cha chini cha Mshahara katika Sekta ya Umma.Balozi Asha Rose Migiro azindua Jumuiya ya Watanzania Waishio Wales, Uingereza

Tarehe 29 APRILI, 2017 Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha Rose Migiro aliwatembelea Diaspora waishio Nchini Wales. 

Katika mkutano wake na Diaspora hao, Balozi alishiriki uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania Waishio Wales (WAWE-TZDiaspora). 

Jumuiya hiyo inawajumuisha Diaspora Waishio katika miji ya Bristol, Bath, Somerset, Wiltshire, Newport, Cardiff na Swansea. 

Katika uzinduzi huo, Balozi aliwapongeza Diaspora wa Wales na Uongozi Wao pamoja na kutoa wito wa kushirikiana kwa karibu na Ubalozi wa London kupitia uongozi wako. Alihimiza umuhimu wa Diaspora kuwa wamoja na kushirikiana bila kubaguana. 

Diaspora hao waliagana na Balozi kwa kumuandalia chakula maalum cha kumshukuru kwa kuwatembelea na kwa heshima aliyowapa kuzindua Jumuiya ya WAWE-TZ Diaspora. 
 .Balozi akizindua Jumuiya ya WAWE-TZ Diaspora kwa kupokea Katiba ya Jumuiya hiyo. 
 Balozi akizungumza na wanachama wa WAWE-TZ 

 Balozi na Uongozi wa Jumuiya ya WAWE-TZ 
Balozi akishiriki chakula alichoandaliwa na Jumuiya ya WAWE-TZ 


UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI VYAINGIZA HASARA TANGA UWASA YA MILIONI 13 KWA SIKU.

Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza. 

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye vyanzo vya maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika maeneo hayo. 


Mhandisi Mgeyekwa alisema shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika. 


Aidha alisema kuwa awali mamalaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya Jiji la Tanga. 


Alisema wao kama mamlaka baada ya kugundua kuwepo kwa tatizo hilo walianza kufanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuvitembelea vyanzo vyote vya maji ili kubaini uhalisi uliopo na namna ya kuanza kulishughulikia jambo hilo kwa haraka zaidi ili lisiweze kuleta madhara kwa wananchi. 


“Ki ukweli tatizo hili la katizo la maji na maji kutoka machafu haliwaathiri wananchi peke yake hata sisi kwenye maeneo yetu tunayokaa limekuwa likijitokeza hivyo tunaangalia namna ya kupambana nalo usiku na mchana kwa lengo la kutatua shida hiyo”Alisema. 


Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akizungumza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu dawa ambazo zinatumika kuwekwa kwenye maji 
Mratibu wa shughuli za Mazingira wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga Tanga Uwasa,Ramadhani Nyambukah akiwaonyesha mitambo iliyopo kwenye kituo hicho wakati walipoitembelea kujionea

Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Citizeni Mkoani Tanga, George Sembony akiwa kwenye vyanzo hivyo vya maji 


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


NAIBU SPIKA TULIA ACKSON AZINDUA MAFUNZO YA SANAA TASUBA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

TAASISI ya Tulia Trust inayomilikiwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson imewafadhili wanafunzi 27 kwa ajili ya kupata mafunzo ya sanaa.

Taasisi hiyo imewadhamini wanafunzi hao kutoka Mbeya kusoma kwenye chuo cha Taasisi ya Sanaa na Utamaduni (TaSUBa), kilichopo Bagamoyo mkoani Pwani.

Wanafunzi hao watapata fursa ya kujifunza sanaa ya maonyesho ya upigaji ngoma za asili, maigizo na utumiaji jukwaa.Akizungumza kwenye uzinduzi wa kuwakabidhi wanafunzi hao chuoni hapo, Dkt. Tulia amesema lengo la kuwafadhili vijana hao ni kutokomeza tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana.

Amesema taasisi yake imedhamilia kukuza sanaa kwa vijana nchini ili kutatua tatizo la ajira na kuongeza ufanisi kwenye vipaji vyao walivyokuwa navyo awali.Alisema vijana hao wakipata mafunzo kwenye chuo hicho wataweza kufanya shughuli zao za ngoma za asili kiutaalamu zaidi, hali itakayowaongezea kipato na kuwafungulia fursa nyingi.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya Vikundi vya  ngoma za asili kutoka mkoa mbeya yanayofadhiliwa na Tulia Trust.

Mtendaji mkuu wa chuo cha Sanaa Bagamoyo(TASUBA) akizungumza kumkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson, akicheza ngoma pamoja na Mtendaji mkuu wa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo , Dk Herbert Makoye.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Tulia Ackson akiwasili katika chuo cha Sanaa Bagamoyo kwa jili ya ufunguzi wa mafunzo kwa vikundi vya Sanaa mkoa mbeya.