Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu), Mhe.
Jenista Mhagama, amewataka wananchi wote kushirikiana na kusherehekea miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania bara
kwa kuunga juhudi za serikali ya awamu ya Tano ya kupinga ufisadi na rushwa
nchini.
“Kwa
niaba ya serikali natoa wito kwa wananchi wote nchini kusherehekea siku hii kwa
kuwakumbuka waasisi wetu waliotetea na kutuletea Uhuru wa nchi yetu.
"Aidha
niwaombe wananchi wote kuunga mkono juhudi za Rais wetu Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli katika kuimarisha uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchi
yetu” amesema Mhe. Mhagama.
Kauli
mbiu ya sherehe za kutimiza Miaka 55 ya uhuru ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga
Rushwa na Ufisadi na Tuimarishe Uchumi wa Viwanda kwa maendeleo yetu”
Mgeni
Rasmi katika Maadhimisho hayo atakuwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Jackson Lyaniva wakati akikagua maandalizi ya maandhimisho ya miaka 55 ya Uhuru Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam tarehe 8 Desemba, 2016 (katikati) ni Mkurugenzi wa Idara ya Maadhimisho na Sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Mazelengwa
Mtumishi katika wa Idara ya Maadhimisho na Sherehe za kitaifa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Hamad Hashim akisafisha zuria wakati wa maandalizi ya maandhimisho ya miaka 55 ya Uhuru Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo tarehe 8 Desemba, 2016.
Nafurahi kuona jamaa hajapiga stop sikukuu hii kama mwaka jana.
ReplyDeleteHii ndiyoitkuwa sherehe ya kwanza ya kitaifa kwa JPM kuwa mgeni rasmi. Rais wetu ameonesha kwamba mambo yakianza kwenda mswano mambo kama haya yana umuhimu wake. Sio wakati ule shida kibao kila kona halafu mnatumia mabilioni ya shilingi kwa khanga na Tshirt. Hongera Rais wetu kipenzi cha wanyonge
ReplyDelete