THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.


Share Michuzi Blog

KIJANI CHATAWALA SEHEMU KUBWA YA MJI WA KILWA, LINDI

Hii ni barabara kuu itokayo Kilwa Masoko kuelekea Nangurukuru, Mkoani Lindi
Kijani kila kona.
Watanzania kunufaika zaidi na Gesi Asilia

·       Iwapo kutakuwepo ushirikishwaji wa wananchi
·       Wataalamu nao watoa yao ya moyoni

KUTOKANA na kugundulika kwa hazina kubwa ya gesi nchini  ambayo inategemewa kukuza pato la taifa zaidi ya mara 15 ya sasa, kiasi cha kuiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

Hata hivyo, dhana ya kwamba Rais ajaye baada ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete kumaliza muda wake, anaweza akaikuta Tanzania ikiwa ni nchi tajiri tayari kutokana na rasilimali hiyo ya gesi asili, inaweza isiwe sahihi kama hautawekwa mfumo madhubuti wa ushirikishwaji wa wananchi katika fursa zilizopo katika rasilimali hiyo, sera, sheria na usimamiaji mzuri wa raslimali hiyo.

Pia itawezekana tu iwapo viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali hiyo watahakikisha wanaisimamia kikamilifu kwa mujibu wa sera na sheria zitakazotungwa na kusimamiwa na viongozi wenye dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania na nchi yao kwanza.

Hayo pamoja na mengine yalijadiliwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Watanzania wapatao 400 kutoka wilaya mbalimbali ambapo walitoa maoni yao kuhusu ni jinsi gani mapato yatakayotokana na gesi yatawanufaisha wananchi wote wa Tanzania.

Dr Abel Kinyondo & Invited Expert Innocent Bash from TEITI addressing the media .
 Expert Mr Dennis Rweyemamu (Head - Policy and Research, UONGOZI INSTITUTE) answering questions
 January Makamba and Mujobu Moyo listening to participants
January Makamba answering questions from participants 
Moderator discussing topics with participants .


RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita (shati jeupe) kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya  Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  
Rais Kikwete akiondoka msibani akiwa ameongozana na mtoto wa marehemu Bw. Iddi Mbita, Balozi Tambwe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. Picha na IKULU


Dar mabingwa mchezo wa vishale "Darts" Taifa

Machezaji wa vishale(Darts) wa klabu ya Friedz ya Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam wakiwa wameshika kikombe mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya mchezo huo yaliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.Friendz walizawadiwa Kikombe na Pesa taslimu Shilingi 100,000/=.
Bingwa wa mchezaji mmoja mmoja (Singles) wa mchezo wa Vishale(Darts), Erry Boates kutoka klabu ya Lugalo akishangilia na kikombe mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Tiptop Manzese jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Balozi Rajabu Hassan Gamaha ateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

 Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
 Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

27 Aprili 2015


Mkutano wa siku mbili wa Mawaziri wa SADC Waanza jijini Harare

Na Mwandishi wa Wizara
ya Mambo ya Nje.
Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) wameanza kikao cha siku mbili jijini Harare, Zimbabwe leo kufanya matayarisho ya Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo, utakaofanyika hapo tarehe 29 Aprili, 2015.
Kikao cha Mawaziri, kinachoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. Simbarashe Mumbengegwi, kinatayarisha agenda ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi, ambao utajikita kwenye Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Viwanda wa nchi za SADC. Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye mkutano huo, utakaofanyika chini ya Mwenyekiti wa SADC, Rais Robert Mugabe.
Katika kikao cha Mawaziri, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, anawakilishwa na Naibu wake, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, ambaye aliwasili Harare jana. Washiriki wengine ni Waziri wa  Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba, Naibu waziri wa Uchukuzi, Mhe. Dkt. Charles Tizeba na Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Gerson Lwenge.
Mbali na mkakati wa maendeleo ya viwanda na mpango wa utekelezaji wake, Mawaziri watajadili Mpango wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Miundombinu na uanzishwaji wa Soko Huria la Utatu baina ya nchi za SADC, EAC na COMESA.
Kikao cha Mawaziri kilitanguliwa na Kikao cha Maafisa Waandamizi, kilichosimamiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajab Gamaha na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Musa Uledi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Zimbabwe, Mhe, Simbarashe Mumbengegwi akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unaojadili Mkakati na Mwongozo wa kuelekea Maendeleo ya Viwanda katika Kanda ya SADC. Mhe. Mumbengegwi amefungua mkutano huo jijini Harare, Zimbabwe  huku akiwa na huzuni kubwa kufuatia taarifa ya kifo cha Bregedia Jenereli Hashim Mbita ambaye alitoa mchango mkubwa katika ukombozi  wa nchi za Kusini mwa Afrika. Mhe. Mumbengegwi aliwaomba wajumbe wote wa mkutano kusimama ili kumuombea dua Bregedia Hashim Mbita.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Abdallah Kigoda (Mb) wa katikati akiomba dua kumkumbuka Brigedia Hashim Mbita. Kulia kwa Mhe, Kigoda ni Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mwigulu Nchemba (Mb) na kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb) nao pia wakimuombea dua Brigedia Jenerali Hashim Mbita.
Meza kuu nayo ikimuombea  Brigedia Jenerali Hashim Mbita. Kwa habari zaidi na picha BOFYA HAPA 


Ulega azindua awamu ya pili ya Kampeni ya uhamasishaji ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Wilayani Kilwa leo

Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdala Ulega amewakata watendaji na watoa huduma wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatina muda wote ili kuboresha huduma wilayani hapo.

Ulega ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa taifa wa bima ya afya katika halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa kata ya Tingi njia nne wilayani kilwa.

Ulega amesema Serikali kupitia mfuko wa uchangiaji wa bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.

Awali, Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Bima ya Afya, Rehani Athumani alimweleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa kampeni hiyo iliyozinduliwa leo itafanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

Rehani alizitaja halmashauri hizo kuwa ni Kilwa, Ruangwa, Ulanga, Korogwe na Rufiji. Nyingine tano ambazo huduma za mfuko wa CHF zitaanzishwa na kuhamasishwa katika kampeni hii ni Halmashauri ya Kaliua, Kakonko, Ushetu na Itirima.

Naye mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga aliwaahidi wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara kuendelea kushirikiana nao katika kutatua changamoto mbalimbali ili kuboresha huduma za matibabu kupitia Mfuko wa Afya wa Jamii katika mikoa hiyo. 

Aliomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.

Hadi tarehe 31 machi, 2015 mfuko wa afya ya jamii ulikuwa umeandikisha jumla ya kaya 930,879 sawa na wanufaika 5,85,274.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilayani Kilwa, wakati uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akielezea namna kampeni hiyo inavyofanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa fedha wa 2014/15, katika uzinduzi uliofanyika leo katika Kijiji cha Njia Nne, Kata ya Tingi wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.
Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mashuka 150 kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani(kulia) kwa ajili ya Zahanati za Wilaya ya Kilwa.


TASWIRA KUTOKA MORO-DAR
YANGA BINGWA 2015,YAINYUKA POLISI MORO 4-1

 Simon Msuva (kushoto) akishangilia na Amis Tambwe baada ya Tabwe kuipatia timu yake bao la katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga imeshida 4-1. (Picha na Francis Dande)
 Mashabiki wa Yanga wakishangilia bao lililofungwa na Amis Tambwe.
 Mshambuliaji Wa Yanga, Simon Msuva akimtoka beki wa Polisi Moro, Hassan Mganga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Shabiki wa Yanga akifurahia bao la pili la timu yake.
 Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya kumalizika kwa mchezona Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
 Amis Tambwe akipokea mpira baada ya kufunga"Hat Trick"
 Kocha wa Yanga, Hans Pluijm akishangilia baada ya timu yake kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.
 Mashabiki wakishangilia.


RAIA WATATU WA KIGENI WAKAMATWA KWA MAKOSA YA WIZI WA MTANDAO KATIKA MABENKI JIJINI DAR ES SALAAM.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa watatu raia wa kigeni kwa makosa yanayohusiana na wizi wa mtandao kwa lengo la kuiba  katika vyombo vya fedha kama mabenki, maduka ya kubadilishia fedha (Bureau de Change) au kuingilia miamala ya fedha zinazosafirishwa na wateja kutoka nje na ndani ya nchi. 

Polisi wa kikosi Maalum cha kupambana na wizi wa mtandao (Cyber Crime) walipata taarifa za kuaminika kwamba watu hao watatu walikuwa katika mazingira ya kutiliwa mashaka na ndipo Polisi walienda Mtaa wa Mindu eneo la Upanga na kuwakamata. Watu hao walikutwa katika nyumba namba 416 iliyopo katika ghorofa ya nne na walitambuliwa kwa majina yafuatayo:

1.    FOTIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 32, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Raia wa nchini UGIRIKI mwenye Passport namba AK2669977.

2.   ATHANASIOS S/O VOGIATZIS, Miaka 30, Mfanyabiashara, Mkazi wa Upanga, Mkazi wa Ugiriki mwenye Passport namba AK3049876.

3.   PANAGIOTIS S/O ANGELIDIS,   Miaka 25, Mkazi wa Upanga, Raia wa UGIRIKI mwenye Passport namba AK2644930.

Watu hao watatu ambao ni raia wa nchini Ugiriki kumbukumbu zao zinaonyesha kwamba wamekuwa wakiingia na kutoka nchini Tanzania na kwenda nchi mbalimbali za Afrika na Ulaya katika namna ambayo inaonyesha kuwa ni wahalifu wa kimataifa kupitia mitandao.

Katika upekuzi watu hao wamekamatwa na vielelezo mbalimbali vinavyopashiria njama zao kama ifuatavyo:
1.    Muhuri mmoja wa kughushi ulioandikwa “Inspector General of Police DSM”

2.   Nyaraka mbalimbali za kughushi za Polisi Tanzania zinazowasaidia  kwa lengo la kupata malipo ya bima nje ya nchi ambazo zina mihuri ya kughushi.

3.   Zimepatikana Kompyuta Mpakato (Laptops) zipatazo tisa ambazo watuhumiwa hawa huzitumia kwa ajili ya mawasilisano pamoja na uhalifu huo wa kimataifa.

4.   Zimekamatwa laini za simu za mkononi (Cheap) za kampuni ya simu ya Airtel ambazo baadhi zimetumika na nyingine hazijatumika.

5.   Aidha, zimekamatwa kadi mbalimbali za benki (Credit Cards) zipatazo 13 zinazotumika kutoa fedha, kuingiza fedha, au manunuzi mengine za ATM.
Pia watuhumiwa hao wamekamatwa na vitabu vitano vyenye kumbukumbu za majina, anwani, pamoja na namba za siri za wateja mbalimbali wa mabenki mbalimbali kutoka nchi za Tanzania, Zambia, Afrika Kusini, Kenya, Uingereza na Nigeria.

Uchunguzi ziadi unaendelea kuhusu raia hao watatu kutoka nchi ya Ugiriki ili kubaini mtandao wao na kugundua matukio mbalimbali ambayo wameyafanya.

TAHADHARI KWA WANANCHI NA WAGENI WENGINE
Pamoja na kuibuka na wimbi hili la wezi wa mtandao bado ni salama kuweka na kutoa fedha katika mabenki hapa nchini. Hata hivyo kutokana na wimbi hili la wizi kwa njia ya mtandao, ni muhimu sasa kuzuia uhalifu wa aina hii kwa ushirikiano kati ya wamiliki wa mabenki  na wateja wao.  

 Jeshi la Polisi linashauri (pamoja na maelekezo mengine ya benki) njia sahihi ya kwanza ya kuzuia ni kuhakikisha kwamba miamala yote inayofanyika katika akaunti za benki ni lazima ifahamike kwa mteja kwa njia zifuatazo:

1.    Mteja ajulishwe kwa simu ya mdomo ili kuthibitisha muamala.
2.   Mteja atumiwe ujumbe kwa kila muamala unaofanyika kupitia ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kumjulisha mteja kiasi kilichotolewa, kiasi kilichoingizwa au makato au maingizo yoyote kwa muda ule ule.

Aidha tunawaomba wananchi waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi na wasikubali kutoa nambari za akaunti zao kwa watu wasiohusika au nambari zao za siri hata kwa mtu ambaye ni ndugu wa karibu sana.
Mara baada ya upelelezi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.

S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.


WAKAZI WA MLONGAZILA WALIVYOVAMIA WIZARA YA ARDHI MAPEMA LEO MCHANA


WAZIRI MKUU PINDA ASISITIZA UWAZI KATIKA MATUMIZI YA TAKWIMU SAHIHI

 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akionyesha kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akizindua kitabu kinachoeleza Maendeleo na historia ya Takwimu katika Bara la Afrika alichokizindua leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Takwimu (ISI) Bw. Vijay Nair na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kushoto kwa Waziri Mkuu na Prof. Ben Kiregyeza (kulia) ambaye ndiye mwandishi wa kitabu hicho.
  Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda akifungua  Kongamano la Kimataifa la Siku 3 la Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika leo jijini Dar es salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa awali akizungumza na Wakuu wa Taasisi za Takwimu wa nchi 38 za Afrika na 18 kutoka nje ya Bara la Afrika waliohudhuria Kongamano la Siku 3 la Kimataifa kujadili Matumizi ya Takwimu leo jijini Dar es salaam.


NMB YAPATA TUZO KWA KUCHANGIA ZAIDI HUDUMA ZA JAMII

NMB imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla katika makampuni ya biashara yanayojali zaidi jamii kwa kutoa sehemu kubwa ya faida yake kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii ya kitanzania.

Ushindi huo umetokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti wa huduma za maendeleo ya jamii - Research Centre for Social Development Services kwa kushirikiana na kampuni mwenza ya konsalt limited imetoa tuzo hiyo kwa NMB baada ya kujiridhisha kuwa ndiyo benki inayoongoza kwa kusaidia jamii zaidi.

NMB imeyapiku makampuni na benki zingine 9. NMB hutoa asilimia moja kwaajili ya kuchangia maendeleo hususani madawati mashuleni, vifaa mahosipitalini, kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kuchangia jamii kipindi cha majanga kwa kuchangia vifaa mbalimbali kwa wahanga.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Mtarajiwa wa NMB Bi. Ineke Bussermaker alisema “NMB imedhamiria mchango kwa jamii sio tu katika huduma za kibenki kwa wateja bali pia kutoa sehemu ya mafanikio yetu ili kuisadia jamii katika maeneo makuu matatu - kutoa elimu kuhusu huduma za kifedha, kuchangia katika sekta ya Afya, misaada mashuleni na mchango kwenye matukio ya maafa”.
 Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB-Bi Ineke Bussermaker akipokea tuzo ya Mshindi wa jumla kama taasisi inayochangia zaidi huduma za jamii kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara -Abdala Kigoda.
Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB - Bi Ineke Bussermaker pamoja na Waziri wa Viwanda-Abdala Kigoda wakipata picha baada ya makabidhiano ya tuzo hiyo.  


WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, LAZARO NYALANDU ATEMBELEA CHUO CHA USIMAMIZI WANYAMAPORI PASIANSI-MWANZA

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akiangalia moja ya kompyuta maalum zinazotumiwa wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa jili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akijaribu akikagua moja ya vitanda na hema linazotumiwa na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akicheza na mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Pasiansi mjini Mwanza alipokwenda kukagua vifaa mbalimbali vilivyonunuliwa na Taasisi ya Buffet Foundation kwa ajili ya mafunzo ikiwemo vitabu, kompyuta, magari na darubini.

HABARI PICHA ZAIDI BOFYA HAPA