Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari WAMA- Nakayama wakionyesha maonyesho ya masomo kwa Mgeni Rasmi, Mhe. Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete pamoja na wageni waalikwa.
Mke wa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akisoma hotuba yake kwa wageni waalikwa na wahitimu wakati wa Sherehe za Mahafali ya kwanza ya Kidato cha Sita ya Shule ya WAMA- Nakayama.
Mgeni Rasmi Mhe. Ummy Mwalimu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto akihutubia wahitimu, walimu na wageni waalikwa wakati wa sherehe za mahafali.
Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya WAMA - Nakayama katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa WAMA mara baada ya kumkabidhi Cheti cha Shukrani kwa mchango wake katika maendeleo ya elimu yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2016

    NICE PIC OF MAMA KIKWETE NA GRADUATES. GOOD JOB. WE MISS YOU FIRST LADY.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 05, 2016

    Someni kina dada mjitayarishe na maisha ya ulimwengu wa sasa hivi. Kujitayarisha kunatakiwa hata kama baadaye utaolewa au hautaolewa jitayarishe kujikimu kimaisha. Wapo wanawake walioachwa wajane na wapo waliotelekezwa katika hali yoyote utakayojikuta nayo ikukute umejitayarisha kuikabili.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 05, 2016

    kwa kufanya wasichana wawe competent tangu nyumbani, shuleni, na kazini na siyo kuwafanya namba 2 (kwa kudhani hawawezi wenyewe pekee eti lazima mtu awashike mkono). Tubadili jinsi tunavyomlea msichana ili ajue yu sawa na mvulana na kwamba anaweza kumshinda mvulana katika kila kitu. Mi huwambia wanafunzi wangu kuwa tofauti ya msichana na mvulana ni kwamba msichana anaweza kujifungua na mvulana hawezi. Ukiacha tofauti hiyo, vyengine hutegemea akili ambazo ni sawa. Mfano, msichana anaweza kupata GPA kubwa zaidi ya wanafunzi woote na pia mvulana anaweza. Tuache kule wasichana kama ni watu wanaosubiri kuolewa, kuachiwa matumizi, kujifungua, kudeki, kufagia, na kufua. Bali, ni watu wataalam, wanaoweza kujenga taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...