Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MASHINDANO ya riadha watoto yanatarajiwa kufanyika Juni 5  huku benki ya Azania wakidhamini mbio hizo na kuzipa jina la Azania Bank Kids Run 2016 ambazo zitakuwa na malengo ya kuwekeza kwa watoto wadogo ambao watakuja kuwa wanariadha wazuri baadae.

Akizungumza kuelekea siku hiyo,Afisa Masoko Muhandamizi Othman Jibrea amesema lengo kuu la kudhamini mashindano hayo ni kuweza kuwajenga watoto wadogo kuweza kuanza kupenda michezo ikiwemo riadha kuanzia umri mdogo na kuja kuwa wanamichezo wazuri watakaoleta tija kwa taifa baadae.

"Malengo ya kudhamini mashindano haya ni kuweza kuwaandaa vijana wadogo kuweza kupenda michezo ikiwemo riadha na yatakuwa ni endelevu na udhamini huu utayafanya mashindano haya kuwa ya uhakika na yenye ubora wa viwango na tunatarajia kuibua vipaji vya riadha nchini,"amesema Jibrea. Mashindano hayo yanatarajiwa kuwashirikisha watoto zaidi ya 2,000 kutoka maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Mbio hizo zitakuwa katika vipengele vitano kwa kushirikisha watoto kuanzia umri wa miaka 2 hadi 17 na mbio ndefu zaidi zitakuwa ni kilomita 5 zitakazoanzia Mnazi Mmoja na kupita katika barabara mbalimbali za jiji la Dar es salaam na kuja kuishia barabara ya Lumumba.

Kwa niaba ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Mjumbe wa kamati hiyo, Tulo Chambo amesema kuwa wamefurahi na kuipongeza benki ya Azania kuweza kuwadhamini katika mbio hizo zitakazokuwa na malengo ya kuinua vipaji kwa watoto na watakuwa na mbio tofauti kuanzia mita 50 hadi kilomita tano na kwa watoto wadogo wa miaka miwili watakimbia nusu uwanja sawa na mita 50.

"Natoa rai kwa wazazi kuwaleta watoto wao siku hiyo katika viwanja vya Mnazi Mmoja na tunategemea kuona wakijitokeza kwa wingi na kuyafanya mashindano haya kufana na kuibua vipaji vipya kwani pamoja na hilo pia tunatarajia mbio hizi kuleta umaarufu nchini hususani kwa Jiji la Dar es salaam kam nchi zingine wanapoyapa majina majiji yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...