Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za serikali/umma, kwa mwaka huu.

Balozi Sefue, ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.

Badala yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba, 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Lets wait,see and tight our belts...This mhe. sounds like the late Sokoine in those days!

    ReplyDelete
  2. LET US PRAY FOR HIM.MUNGU ATASIMAMA NAE.

    ReplyDelete
  3. Kimaadili, JPM kapatia kabisa. Serikali ya kisecular kusherehekea dini offisini haviendani. Dini ni ya moyo wa mtu binafsi akafanyie kwenye nyumba za ibada au nyumbani kwake.

    Serikalini kazi tu.

    HAPA KAZI TUU.

    NAKWAMBIA KATIBA IBADILISHWE ILI TUWE NAYE MUDA MREFU. AKIONDOKA KUMPATA MWENGINE WA HIVI IKO KAZI.

    HUYU NDIYE RAISI WA WOOTE. NA KWENYE DINI YAKE SIHISI KAMA NI DHAMBI KUWA MWADILIFU KIASI HIKI.

    ReplyDelete
  4. Huyu jamaa anatekeleza kiapo kama kilivyo. Anatuonyesha anaaminika, ni mwaminifu, na mwadilifu. Wangekuwa wengine wangeogopa dhambi kwa kukinza dini ambavyo ingekuwa kosa. Fedha za serikali ni kodi za watu wenye dini na wasio na dini. Kuruhusu waajiriwa wa dini moja kutumia fedha hizo bila mgawo kwa watu wa dini nyengine na wasio na dini ingekuwa dhuluma japo usoni laonakana ni zuri kwa sababu kuna sala. hela ya dhuluma haifai kutoa sadaka hata ikiombewa baraka haibarikiki.

    JPM, aagize somo la maadili (ethics) kuanzia darasa la kwanza mpaka phd. na serikali isiajiri asiyesoma somo hilo.

    ReplyDelete
  5. Mimi nasubr tu siku akitoa agizo la kufuta mbio za mwenge maana sioni faida zaidi ya kuliingizia taifa hasara

    ReplyDelete
  6. Sajitahidi lakini sababu sio nzuri.

    Sababu ya kubana matumizi ni ya kiuchumi na si ya kimaadili yeye akiwa mwana-maadili.

    Sababu ya kimaadili ni kwamba si vizuri kwa waajiriwa wakristo kutumia fedha za serikali ya kisecular kwa sababu za kidini bila kuwepo mgawo sawa kwa wasio na dini na kwa watu wa dini nyengine, wa....n.k.

    ReplyDelete
  7. kweli kabisa naomba sana afute sherehe zote pesa za kushereheka kumbe watu wanafanya ndio maisha yao kwa kutuumiza sie wanyonge kufuja kodi tunazolazimishwa kutoa sie walalahoi haileti maana, mifisadi inanehemeka kwa kutunyonya haki zetu, naomba sana Rais wetu futa kabisa sherehe zote mtu akitaka kushereheka akasherekee kwake kwa pesa yake na sio kutunyonya sie.mapesa mengi yanapolwa na mafisadi kwa visingizio sherehe za serikali upuuzi mtu hayo mafungu ya pesa yapelekwe mahospitalini na mashuleni. Pongezi kwa sana kwa Rais wangu Magufuli na Mungu awe nguzo yako kwa kila jambo - Amen

    ReplyDelete
  8. St Augustine University of Tanzania (SAUT) wana somo la ethics....vyuo vingine muige hilo

    ReplyDelete
  9. Hivi kumbe serikali ilikuwa na fungu la krismasi kwa waajiriwa? Nimefumbuka macho nlikuwa sijui.

    Fungu la Eid na Maulid liko wapi. Au lipo muheshimiwa anaogopa kusema. Nalo lisiwepo.

    Huyo ni mkristo mwadilifu. Hajafanya dhambi wala hachukii krismass bali anataka haki. Anayeona kakosea basi ajuwe ana tatizo la kimaadili na huenda akaenda jehanam hta kama anasali.

    ReplyDelete
  10. Hivi fungu la krismas lilikuwepo kwa sheria au katiba ipi.

    JPM liweke hili wazi na data kabisa ni bilioni ngapi. Manake we mzee wa data.

    ReplyDelete
  11. Allaah kawajaaliya urais Mwinyi na Kikwete lakini walishindwa kuleta usawa. Leo kaja mkristo mpenda maadili kazi ya wiki tatu ni kubwa zaidi ya miaka 20.

    Kama Negus wa Ethiopia wakati wa Mtume. Masahaba wamepigwa wakaokolewa na mkisto mwana maadili.

    Wako wachache akina JPM. Wengine kusali tu ndo dini kwao na sio uadilifu.

    ReplyDelete
  12. Somo la ethics likifundishwa tutapata akina JPM wengi na kutakuwa hakuna haja ya kubadili katiba.

    Lakini kama somo hilo hamna basi katiba itoe exception kwa watu nadra kama JPM.

    ReplyDelete
  13. Ufisadi umekithiri kana kwamba mioyo ya waumini imekuwa kipofu na kuliona jambo la kawaida.

    Angalia waumini wanatumia kwa sababu za ki-roho fedha iliyozalishwa kwa ajili ya matumiazi ya umma (elimu, afya, ulinzi, ustawi, nk.) bila ya waumini hao kuona tatizo kwamba ni fadha za kudhumu uma. Tena huenda ndo wanaona huyu JPM nuksi. Ukiona JPM nuksi ujuwe una tatizo la ki-roho maana anachofanya ulitakiwa kukifanya wewe kabla yeye hajawa rais.

    Hivi hicho chakula katika tafrija ya krismass kwa fedha za umma Mungu atakibariki vibi? Kwa sababu tu baraka zimeombwa? Au hizo sala zitakubilika vipi kwa Mungu wakati nguvu za kusali zimetokana na matumizi mabaya ya fedha za umma?

    ReplyDelete
  14. USHAURI

    JPM au wabunge waadilifu waandike muswada wa kanuni za serikali kufadhili tasisi za kidini au zenye ufungamano na dini.
    1. taasisi moja ikipewa ruzuku basi taasisi nyingine mithi yake kwenye dini nyengine zitaitwa kupewa fair-share na rais lazima atangaze bungeni na kwenye gazeti la kiserikali.
    2. Pasiwepo na MOU yeyote kati ya serikali na taasisi moja kisiri bila ya taasisi nyengine kujuwa na pia taasisi nyengine zipewe fursa sawa ya MOU na faida hizo.
    3. Serikali ikiipa hadhi, fursa, au nafasi taasisi moja basi na nyengine mithilye zitakaribishwa kupokea mithilizo.

    usishangae atayeweka pingamizi ni muumini. utashangaa dini ziko kwa ajili gani sasa kama hazisaidii kumfanya muumini awe mwadilifu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...