Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashine mojaya Ventilator  ya kumsaidia mgonjwa kupumua yenye thamani ya Dola za Kimarekani 36,000  sawa na Shilingi milioni 80.

Msaada huo umetolewa leo na Kituo cha kitabibu cha Halmiton chenye makao yake makuu nchini Switzerland .

Akikabidhi mashine hiyo  mpya na  kisasa , Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika kutoka Halmiton , Qasem Sumrein amesema pamoja na kutoa msaada huo wataendelea kutembela MHN ili kutoa mafunzo jinsi ya kuitumia pamoja kufanya matengenezo endapo itahitajika kwa kuwa mashine hiyo ina waranti ya miaka miwili.

Akipokea msaada huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MHN, Profesa Lawrence Mseru ameshukuru msaada huo ambao una lenga kuboresha huduma za afya na kueleza kwamba hospitali hiyo inahitaji kutengeneza ICU nyingine ikiwamo ya mama na mtoto hivyo bado zinahitajika mashine 120 kwa sababu MHN inapokea wagonjwa wengi.


Akielezea  kuhusu mashine hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Usingizi Moa Kalunga amesema  mashine hiyo itamsaidia mgonjwa aliye mahututi kupumua na hivyo kuokoa maisha yake na mgonjwa akirejea katika hali ya kawaida mashine hiyo  inaonyesha .
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akipokea mashine ya ventilator ya kusaidia wagonjwa kupumua endapo wamezidiwa baada ya kuugua. Kushoto ni Mkurugenzi Mauzo wa Mashariki ya Kati na Afrika, Qasem Sumrein akikabidhi mashine hiyo leo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN), Profesa Lawrence Mseru akitoa ufafanuzi baada ya kupokea mashine hiyo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa Mahututi na Uzingizi, Moa Kalunga katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akiwaeleza waandishi wa habari umuhimu wa mashine hiyo kwa wagonjwa.
Meneja Mauzo barani Afrika, Gordon Blair akimalizia kufunga mashine ya ventilator ambayo imekabidhiwa leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mungu ni mwema kwetu.ukombozi umekaribia

    ReplyDelete
  2. HIVI HATA MASHINE KAMA HIZO HOSPITALI ZA HUKO KWETU BONGO ILIKUWA HAINA?, KWELI HAYO MAJANGA

    ReplyDelete
  3. HOSPITALI ZETU HAZIKUWA NA VENTILATOR HALAFU WATU WAKIFA MNASEMA WAMELOGWA. KWELI SEKTA YA AFYA IPO NYUMA KWELI, MUHIMBILI ILITAKIWA IWE NA MASHINE KAMA HIZO 200 AU ZAIDI LAKINI TUNATEGEMEA TUPEWE MSAADA WA MASHINE YENYE THAMANI YA DOLLAR 2000.......KWELI JAMANI HIZO MASHINE ZIMESHINDWA KUNUNULIWA NA SERIKALI YETU NA KUWEKWA HADI VITUO VYA AFYA????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...