Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefanya ziara ya kushtukiza katika kituo cha afya Kambarage mjini Shinyanga ili kujionea hali halisi jinsi huduma zinavyotolewa kwa wananchi siku moja tu baada ya muuguzi wa kituo hicho kukamatwa kwa tuhuma ya kuiba dawa za serikali.Pichani ni mkuu wa wilaya Josephine Matiro na katibu tawala wa wilaya ya Shinyanga wakiwa katika chumba cha kuhifadhia dawa wakiwa wamepigwa butwaa baada ya kuona chumba kimesheheni dawa wakati mara kwa mara wananchi wamekuwa wakiambiwa hakuna dawa badala yake wanaambiwa wakanunue kwenye maduka ya watu binafsi mtaani-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Hapa ni ndani ya ofisi ya mganga mkuu/msimamizi wa kituo hicho ambapo mkuu wa wilaya akiwa ameambatana na maafisa wengine wa manispaa ya Shinyanga amekutana na uongozi wa kituo hicho pamoja na wananchi waliomkamata muuguzi mkunga wa kituo hicho Joseph Nkila akituhumiwa kuiba dawa za serikali.Kulia ni Rashid Shaban akimweleza mkuu huyo wa wilaya jinsi walivyofanikisha kufichua wizi huo Wa pili kutoka kulia ni msimamizi wa kituo cha afya Kambarage Dkt Nassoro Yahya akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga kuhusu suala la upungufu wa dawa katika kituo chake ambapo alisema kituo kina upungufu wa dawa na walishatoa taarifa panapohusika siku nyingi zilizopita.

Hata hivyo maelezo yake yalipingana na yale ya kaimu mganga mkuu wa manispaa ya Shinyanga Dkt Mhana Raphael(mwenye suti pichani) aliyedai kuwa mkoa wa Shinyanga hauna tatizo la upungufu wa dawa bali dawa pekee ambayo haipo ni ile ya Antibiotic.
Kwa picha na habari zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Jamaa wa pic ya kwanza kushoto kwa dc lazima atakuwa na udugu na kingwendu asee, dih

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...