Na John Gagarini, Chalinze
Mwanasiasa mkongwe nchini na mwenyekiti wa chama cha Democratic Party mchungaji Christopher mtikila (62)  amefariki dunia jana baada ya gari alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka.
Ajali hiyo ilitokea oktoba 4 majira ya saa 11:45 alfajiri huko chalinze kijiji cha msolwa kata ya bwiringu wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani barabara ya kuu ya Dar es salaam-Morogoro.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani hapa Jafary Ibrahim alisema kuwa katika tukio hilo  watu wengine watatu walijeruhiwa.
"Marehemu na wenzake walikuwa wakitokea mkoani Njombe kuelekea jijini Dar es salaam wakitumia gari aina ya Toyota Corolla lenye namba za usajili t 189 AGM  ambapo alisema liliserereka umbali wa kama mita 150 hadi 200 na kupasuka kioo cha mbele na kusababisha kifo chake," alisema Ibrahim.
Kamanda Ibrahim alisema kuwa watu waliojeruhiwa ni dereva wa gari hilo George Steven (31) maarufu kama ponera mkazi wa mbezi, Patrick Mgaya (57) Ally Mohammed (42) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam ambao wamelazwa kwenye hospitali ya tumbi.
Aidha alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi ambapo gari hilo liliharibika kwa kioo cha mbele na nyuma kutoka pamoja na matairi kupasuka.
Baadhi ya watu walisema kuwa baada ya ajali hiyo kutokea abiria hao walikosa msaada kwani eneo hilo halina makazi ya watu.
Wakati huo huo wananchi wengi wameelezea masikitiko yao kwa vitendo vya watu wengi kurusha picha ya mwili wa marehemu Mchungaji Mtikila ukiwa umelazwa pembeni ya kinachoonesha ni gari alilokuwa akisafiria kabla ya kupata ajali.
Wengi waliowasiliana na ofisi zetu wameitaka TCRA kuwa wakli na sheria zilizopo na ambazo tayari zimeshaanza kutumika zitumike na zioneshe zinatumika".
Kwa kweli inatia uchungu sana kuona badi ya Watanzania sijui kwa ujuaji sana ama kwa kutaka sifa kwenye magurupu huko wamerusha picha ya mwili wa Mch. Mtikila.
"Nimeiona na sikupendezwa nayo kabisa", amesema Benjamin Mbozila akiwa jijini Nairobi. "Afadhali wangerusha ile ya gari tu, lakini mwili mzima na sura inaonekana sio sawa kabis", Janeth Mtonyi alieko ujerumani ametuandikia. Pichani chini ni mabaki ya gari alilokuwa akisafiria Marehmu Mchungaji Mtikilia na abiria wengine watatu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mungu ailaze roho yake mahali pema. Ametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya siasa nchini.

    ReplyDelete
  2. Mola amlaze pema peponi anapostahili, amughufirie kwa yote - AMEN.
    Nadhani suala la watu kuwa wepesi na haraka sana kutuma mitandaoni matukio mbali mbali mara yanapotokea ama kuyashuhudia, ifike wakati tuwe na ule UTU, UUNGWANA na khasa UBINAADAM. Mathalan hili la Mchungaji mtikila inasikitisha sana kuona in a minute, just a click picha za mwili wake tayari keshakata roho, in a second, tayari zimeshazunguka na kuwafikia watu mbali mbali takriban dunia nzima, Jamani iwapi stara ya binaadamu mara umauti unapomfika? Nadhani ni vyema tukazingatia maadili yetu kijamii na kiiimani na kujiwekea mipaka kwa baadhi ya mambo na kufaham miiko na taratibu zake, kwani si kila tukilo ni la kulishadidia au kulichukulia kirakhisi kama tangazo la biashara, leo awe mzazi wako utajiskiaje kuona mwili wake hali ya kuwa ni maiti na ndio kwanza umauti umemkuta, unasanifika mithli hiyo kupitia mitandanoni na sehem nyingine mithili ya hizo? Afadhali basi ingekuwa ndio tayari kwa kumtolea heshima zake za mwisho, lakini ndio kwanza ajali imetokea tu, hili pia tujikumbushe hata Marehem Capt. John Komba, jambo hili pia lilijitokeza, jamani ifike wakati tuwe waungwana wenye kujali utu, ubinaadamu, thamani na hadhi yake na khasa anapokuwa katika taswira nyingine ya umauti/maiti. Rest In Peace Mchungaji Mtikila.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mimi SINA chama cha Siasa ila namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuletea Mchungaji Mtikila kwa maana amesaidia kwa dhati kuleta maendeleo hapa nchini kwa kupambana na Serikali kwa hoja zenye msingi; Kupambana na vyama vingine; nk ambapo harakati zake kwa namna moja au nyingine ziliweza kuamsha Serikali; Chama tawala na vyama vingine na kuleta maendeleo hapa nchini ata kama na yeye alikuwa ana mapungufu kama binadamu wa kawaida na Siasa zake.

      Daima utakumbukwa kwa mengi Mchungaji ukiwa kama Binadamu wa kawaida na utakumbukwa kwa Siasa zako hapa nchini.

      Naomba mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu Mtikila mahali pema peponi; amsamehe makosa na dhambi zake na Siku ya mwisho amkumbuke katika ufalme wake wa Mbinguni.

      Delete
  3. SIKUPENDA KABISA WATU WALIOTUMA HIZO PICHA., WAMENIBOA SANA. LAKINI NAJIULIZA... KWENYE MAKOSA YA MITANDAONI, HII INAANGUKIA KATIKA KIFUNGU GANI? TUSIJE CHUKUA HATUA KUMBE BADO SHERIA IKO SILENT

    ReplyDelete
  4. Utu kwanza kabla ya chochote jamani. Mimi sio mwanasheria lakini hili linanikera sana na sielewi tufanye nini kupitia sheria za mitandao kulikemea na kuwaadhibu. Nimehudhuria misiba kadhaa inafika wakati inabidi itangazwe watu wasipige picha mwili wa merehemu. Hivi hii inahitaji PhD kujua kuwa si sahihi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...