Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar kuhusiana na matokeo ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari (hawapo pichani), ndani ya Idara ya Habari MAELEZO,mapema leo jijini Dar na pia akiwa ameambatana na baadhi ya
Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai (hayupo pichani) ambapo leo wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni 10 kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari ZA Ukimwi (AJAAT), Adolf Simon Kivamwo kutokana na kusumbuliwa na Kansa ya Utumbo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Milioni Tano kwa aliyekuwa mwandishi wa magazeti ya Habari leo na Daily News ambaye alipata ajali  na kumsababishia ulemamvu,Athman Khamis .

 
Waandishi wa habari watatu, Adolf Simon Kivamwo, Athumani Hamisi na Danstan Bahai wamekabidhiwa jumla ya TZS 20m/- kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu  yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Harambee ya Kuwasaidia waandishi wanaougua maradhi mbali mbali, Bw. Benjamin Thompson alisema kuwa fedha hizo ni matunda ya harambee ya Media Car Wash for Cancer Campaign, inayoendelea nchini.

Kama tujuavyo, kwa kuanzia, wanahabari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wengine waliosha magari kwenye viwanja wa Leader Club Julai 4, 2015.

Alisema katika harambee hiyo jumla ya 31m/-, zilipatikana, ambapo kati ya fedha hizo, ndizo wagonjwa wamegawiwa.

“Malengo yetu ya awali yalikuwa kwamba tuwachangishe fedha kwa ajili ya wenzetu wagonjwa, pia kiasi kingine kitumike kuwaingiza baadhi ya wanahabari kwenye mifuko rasmi ya Bima ya Afya. Na ndivyo tulivyofanya leo hii,” alisema.

Bw Thompson alisema kiasi kilichosalia kitatumika kuwaingiza waandishi wa habari 100 katika mpango wa kulipia matibabu kupitia mfuko wa Bima ya Afya, yaani  NHIF.” Alisema.

Alisema lengo la harambee hiyo ni kukusanya jumla ya 100m/- kabla ya mwezi Disemba 2015 na kazi yake kubwa itakuwa kuwahudumia wanahabari wasiojiweza kwa sababu ya kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.

Pia pesa zitokanazo na harambee hiyo zitasaidia kuanzisha mkakati wa mkubwa wa kuhakikisha wanahabari wote nchini wanaingizwa kwenye mfuko wa Bima ya Afya.

“Lengo letu ni kuhakikisha wanabari wana kinga za afya zao,ili tukomeshhe huu mtindo wa kuchangiana mara kwa mara kila mmoja anapougua,”alisema na kuongeza kuwa  watakaohusika katika zoezi hilo, ni wale wasioajiriwa pamoja na wasioajiriwa lakini hawana huduma ya Bima ya Afya.

Ili kuendeleza mchakakato wa kufikia lengo kuu, wanahabari Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na wenzao wa Jijini Dar es Salaam, Agost 15 mwaka huu, wataosha magari kwenye viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza.

Tunaomba wadau mbalimbali waungane nasi kwenye hili,ikiwemo kulipia gharama mbalimbali ukiwemo usafiri kwenda na kurudi Mwanza,hoteli, matangazo ya radio na mabango.

Wakati huo huo Bw Thompson amesema kutakuwa mkutano wa wadau habari Jumamosi Agost 1, mwaka huu utakaofanyika Msimbazi Centre Jijini Dar es Salaam kwa jili ya kuanzisha mchakato wa usajili wa rasmi wa kampeni hii.

“Tunaomba wanahabari wote nchini watakaoweza kuhudhuria wasikose kufika, maana hapa ndipo juhudi za ukombozi wa kiafya kwa wanahabari zitakapoanzishwa rasmi,” alisema.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisema kuwa Kamati yake imewashirikisha wahariri wote nchini katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na kwamba viongozi hao wa vyumba vya habari ndio waliotoa majina hayo kwa kamati.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...