WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania
wote nchini wajenge tabia ya kuandika wosia ili kuondoa matatizo ya mirathi
pindi mume anapoaga dunia.
Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Mei 29,
2015) wakati akizindua kampeni ya kuandika wosia kwenye maadhimisho ya miaka 25
ya Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) yaliyofanyika katika viwanja
vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
mara baada ya kushuhudia uandishi wa wosia mbele ya wakili, Waziri Mkuu alisema
uandishi wa wosia ni suluhisho la migogoro mingi inayosababishwa na wanandigu
ambao wakati mwingine wala hawakushiriki kuchuma mali wanayogombea.
“Kuandika
wosia siyo uchuro kama ambavyo watu wengi wanadhani… ninatoa kwa Watanzania
kuandoak wosia mapema kwani inasaidia kuondoa matatizo ya mirathi baada ya
mmoja wao kuondoka duniani,” alisema.
“Mtua
anapaswa kutamka mali nilizonazo ni kadhaa na endapo nitakufa mali hii apewe
fulani, na hii fulani na nyingine fulani. Hati hii inapaswa kutunzwa kwa
mwanasheria, benki au kwa Kabidhi Wasii. Tusipolifanya hili, matatizo
yataendelea kuwakumba wajane na watoto walioachwa na marehemu,” alisema.
Aliipongeza
TAWLA kwa kuchukua jukumu la kuhamasisha umma kuhusu suala la uandishi wa wosia
lakini pia akawataka wanachama wa TAWLA wajikite zaidi kwenye kutetea haki za
makundi maalum kama walemavu wa ngozi, vikongwe na watu kutoka makabila
madogodogo. “Haya makundi yana shida zao ambazo hazifanani na watu wengine. Nendeni
vijijini, mkatoe elimu, jueni changamoto wanazokabiliana nazo, wasikilizeni
shida zao na muone ni njia gani mnaweza kuwasaidia,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...