Nchini Tanzania watu 147 wamethibitika kuwambukizwa ugonjwa wa homa ya kidinga popo yaani homa ya dengu huku mtu mmoja akiripotiwa kufariki dunia kwa ugonjwa huo.
Kasi ya ugonjwa huo ambao ikiwa hautadhibitiwa unaweza kuleta madhara dalili zake zinashabihiana na zile za malaria kwani unaambukizwa kwa kupitia mbu na unadaiwa kusambaa katika maeneo mengine nchini Tanzania ingawa kwa sasa uko zaidi mjini Dare salaam.
Taarifa zinasema kuwa kuna visa vya wagonjwa nchi jirani ya Msumbiji taifa linalopakana na mkoa wa Mtwara jambo linalozua wasiwasi wa kuwa na visa vingine mkoani humo. Kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania Joseph Msami amezungumza na Dk Janet Mgamba ni kaimu mkurugenzi msaidizi wa udhibiti na ufuatailiaji wa magonjwa ya milipuko ambaye anaanza kwa kueleza hali ya kidinga popo ilivyo.
(SAUTI MAHOJIANO)
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA
kidinga popo ndio homa gani? naomba mtuwekee kwa kiingereza au lugha ya kitaaluma.
ReplyDeleteHe! homa hii ni hatari sana, mimi jirani yangu ameipata, ila kwa kuwa alisafiri kwenda nchi za Asia ambamo homa hii ipo kwa wingi nikajua kaitoa huko, kumbe inawezekana kaambukizwa hapa hapa nchini, balaa.Magonjwa yanazidi kuongezeka, Mungu tuhurumie watanzania.
ReplyDeleteNadhani hapa wengine tunahitaji jina la kitaaluma. ndio¨homa gani hii? Kama ugonjwa hatari unazuka nchi jirani nadhani solution ni kufunga mpaka na nchi husika, kuzuia muingiliano.
ReplyDeleteNi Dengue Fever
ReplyDeletesomeni mpaka chini msikurupuke tu.wavivu wa kusoma.
ReplyDeleteKitaalam inaitwa DANGUE FEVER
ReplyDelete