Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, DODOMA

Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO Dkt. Hassan Abbas amesema Sekta ya habari inawajibu wa kupongeza mafanikio ya Serikali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kisasa, elimu bila malipo, ununuzi wa dawa pamoja na ununuzi wa ndege kubwa za kisasa.

Dkt. Abbas ameyasema hayo leo Mjini Dodoma wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari vilivyopo Dodoma ambapo leo ametembelea Redio A.FM na Nyemo FM kwa lengo la kuona na kujua changamoto za kiutendaji wanazokutana nazo pamoja na jinsi gani wamejipanga juu ya ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kutokana na matukio mengi ya Serikali kufanyika Mkoani humo.

“Serikali inapaswa kuungwa mkono, yapo mambo mengi ya kimaendeleo ambayo yanatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano katika sekta mbalimbali ila vyombo vyetu vya habari havitekelezi wajibu wake”

“Sisi kama vyombo vya habari tunawajibu wa kupongeza kwenye mafanikio, kama kuna watendaji wa Serikali wanakosea basi wakosolewe kwa kusema ukweli, hakina staha pale penye mapungufu na sio kwa kukejeli” amesisitiza Dkt. Abbas.

Aidha, Dkt. Abbas amevitaka vyombo vya habari mkoani humo kubadilika katika uandaaji wa vipindi wanavyo virusha kwa kuanza kuandaa vipindi vitakavyogusa mikoa yote na si Dodoma peke yake.“Dodoma sasa inawageni ambao ni watumishi wa Serikali zaidi ya 3000 kwa hiyo na wao wangependa kusikia habari na nyimbo za makabila yao kutoka kwenye redio zenu hivyo yawapasa kubadili utendaji kazi wenu” ameongeza Dkt. Abbas.

Vilevile amevitaka vyombo hivyo kuandaa vipindi vinavyohamasisha wananchi kufanya kazi, kulipa kodi pamoja na kuwaeleza wana thamani gani katika nchi.Kwa upande wake Meneja wa redio A.FM Tatenda Nyawo amesema kuwa redio Afm ipo katika harakati za kuongeza masafa ya redio hiyo kwa lengo la kupanua wigo wa matangazo yao kitaifa ili mikoa mingine iweze kupata habari mbalimbali kutoka Makao Makuu ya Nchi.

Mhariri wa A-fm Regina Mndeme ameongeza, “redio Afm tumejipanga vizuri kuhusu ujio wa Serikali kuhamia Dodoma kwa kufanya kazi kwa weledi na kutangaza rasimali zilizopo mkoani hapa”.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifanya mahojiano katika Kituo cha redio A Fm cha mjini Dodoma wakati wa ziara yake yakutembelea vyombo vya Habari Mkoani humo .
Meneja wa Kituo cha redio cha A Fm cha mjini Dodoma Bw. Tatenda Nyawo (kushoto) akisisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake katika Ofisi za Kituo hicho mapema leo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akifurahia jambo nammoja wa wamiliki wa Kituo cha redio cha A fm Bw. Emmanuel Rutagonya wakati wa ziara yake katika Ofisi za Kituo hicho mjini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watumishi wa Kituo cha redio Afm cha mjini Dodoma mara baada ya ziara yake katika kituo hicho.
Meneja wa Kituo cha redio Nyemo Bw. Hezron Mwandambo (kushoto) ya mjini Dodoma akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa ziara yake katika kituo hicho mapema leo.


Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi Dkt. Hassan Abbasi akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha redio Nyemo ya mijini Dodoma.(Picha zote na Frank Mvungi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...