NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, ameishukuru TANESCO kwa msaada wake wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkoani Mjini Kibaha.

Mhandisi Ndikiro alisema, hatua hiyo yaTANESCO ni ushahidi tosha wa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma afya katika mazingira ya usafi.

"Niseme tu mlichokifanya ni kitu kizuri sana, na ningeshauri taasisi nyingine za umma na binafsi, kutoa sehemu ya faida wanayopata kutokana na shughuli zao na kurudisha kwa umma kwa njia ya kusaidia shughuli za kijamii kama hii ya usafi." Alisema.

Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi Leila Muhaji alisema, TANESCO kama mtoa huduma ya umeme kwa Wananchi na ikitambua kuwa wananchi ndio wateja wake wakubwa, pia imeona ni busara kusaidia serikali katika kuhakikisha mazingira yanayowazunguka kama vile kituo hiki cha afya yanakuwa safi." Alisema.

Bi. Leila pia alisema, TANESCO imetoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha umma kufanya usafi wa jumla kila mwisho wa wiki. "Tumeungana nanyi leo Jumamosi ambayo ni siku ya usafi, ili tufanye usafi pamoja kwenye kituo chetu hiki cha afya, kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, napenda muwashukuru sana na mpokee msada wetu huu mdogo ambao nina hakika utasaidia kwa sehemu fulani katika kuweka mazingira ya hospitali yawe safi." alsiema

Awali Mkuu wa Mkoa Mhandisi Ndikiro, aliwaongoza watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Pwani na wachache kutoka makao makuu katika zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwa kufyeka nyasi kuzunguka mazingira ya kituo hicho cha afya.
Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikiri, (kulia), akipeana mikono na Kaimu Meenja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Bi. Leila Muhaji, wakati akipokea msada wa vifaa vya kufanyia usafi kwa ajili ya kituo cha Afya Mkoani mjini Kibaha Aprili 29, 2017.
Mhandisi Ndikiro, akiwa na Mganga Mkuu wa Mji wa Kibaha, akitoa hotuba yake
Bi leila Muhaji, (katikati), akitoa hotuba yake, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikiro, na Meneja Rasilimali watu TANESCO mkoa wa Pwani, Bi.Nisile Mwakalinga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...