Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili ( MNH),  Profesa  Lawrence Museru  leo amekutana na wahudumu  wa  Afya  katika  hospitali hiyo pamoja na mambo mengine  amewasisitiza kufanya kazi kwa bidii na kwamba uongozi wa hospitali hiyo utaendelea kutatua changamoto zinazowakabili.

Pia, mkurugenzi huyo amewataka wahudumu hao kuzingatia maadili ya kazi  ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa.Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  na baadhi ya wahudumu wa afya  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.

Profesa Museru  amesema licha ya wahudumu hao kukabiliwa changamoto mbalimbali , lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii kwani jukumu lao ni kutoa huduma bora.

" Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayofanya hatua ambayo imesaidia kupunguza malalamiko wakati wa kutoa huduma , ingawa bado kuna changamoto lakini hatua budi kutoa huduma bora  na sisi tutaendelea kutatua changamoto hizo kadiri inavyowezekana  ili kuhakikisha mazingira yetu ya kazi yanakua bora," amesema Profesa Museru.

Katika mkutano huo wahudumu hao wamewasilisha ajenda  14 ikiwamo ombi la kupatiwa mafunzo  ili kuongeza  ufanisi na kuboresha utendaji kazi wao. 
Mwenyekiti wa TUGHE, Tawi la Muhimbili, Mziwanda Salumu Chimwege akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru zawadi kutoka kwa wahudumu wa hospitali hiyo leo.
 Wahudumu wakifuatilia jambo kwenye mkutano huo leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akifafanua jambo kwenye mkutano huo.  Kulia ni Mkurugenzi wa Uuguzi, Agnes Mtawa wa hospitali hiyo.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...