Katibu Tawala wa Wilaya,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo ya Wilaya Ndugu Nyakia Ally,amefungua mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba,huku akiwasihi vijana kucheza mpira wa miguu wakitambua kuwa kwa sasa ni ajira inayolipwa kwa pesa nyingi kulinganisha na michezo mingine hapa nchini.  

 Ndugu.Nyakia alieleza kuwa mashindano hayo yameandaliwa na Diwani wa Kata ya Chemba, Mhe Joseph Saini ambapo yanashirikisha timu sita kutoka katika Vijiji vitatu vinavyounda Kata ya Chemba.

Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya Mbuzi beberu,Katika mashindano hayo yatakayokuwa ya kusimumua wilayani humo,Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally ameahidi kuongeza zawadi ya mipira miwili kwa mshindi wa kwanza, mpira mmoja kwa mshindi wa pili na watatu. 

 Vile vile Katibu Tawala huyo aliwataka vijana kushirikiana katika mashindano hayo bila kujali Itikadi zao za kisiasa, dini wala rangi kwani michezo hujenga Udugu, urafiki na upendo miongoni mwa wapenzi wa michezo husika.

Pamoja na hayo Ndugu Nyakia amemtaka Afisa Utamatuduni wa Wilaya hiyo kushirikiana na Waratibu wa mashindano hayo ili kupata timu nzuri miongoni mwa wachezaji wanao shiriki ligi hiyo,ili hatimaye kupata wachezaji watakao kuwa waanzilishi wa timu ya Wilaya ya Chemba, ili siku za usoni washindane na Wilaya nyingine za hapa Dodoma na baadae Kitaifa na kimataifa kwa kushiriki Soka la kiushindani katika ligi mbalimbali. 
Baadhi ya Washiriki na Washabiki wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye ufunguzi wa mashindano ya Diwani Cup wilayani Chemba mapema leo,ambapo mashindano hayo yamefunguliwa rasmi na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,ambaye ni Mweyekiti wa kamati ya michezo,Ndugu Nyakia Ally (hayupo pichani).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...