Tanzania inakuwa nchi ya 50 barani  Afrika kufikiwa na Shirika la Ndege la Uturuki baada ya kuongezwa safari tatu kwa wiki kwenda Zanzibar

Shirika la Ndege la Uturuki limeiongeza Zanzibar katika mtandao wa safari zake kuanzia Desemba 13, 2016. Hivi sasa shirika hilo linafanya safari 49 barani Afrika baada ya hivi karibuni kuongeza safari ya kwenda Visiwa vya Shelisheli.

Shirika hilo maarufu barani Ulaya kwa sasa linafanya jumla ya safari 293 duniani kote, zikiwemo safari 50 kwenye nchi 31 za Afrika.

Likiwa ni shirika la nne kwa kuwa na mtandao mkubwa wa safari duniani kote kuliko mashirika mengine, Shirika la Ndege la Uturuki sasa litahudumia miji ya kimataifa 244 ikijumlishwa na Visiwa vya Zanzibar ambavyo ni maarufu kwa biashara ya viungo. Watumiaji wa ndege za shirika hilo sasa watafurahia uzoefu watakaoupata kutokana na safari hizo mpya zinazojumuisha miji 20 maarufu duniani kama vile Frankfurt, Muscat, Munchen, Dubai, Paris, London, Milano, Amsterdam, Zurich, Bombay, Copenhagen, Stockholm, Rome, Brussels, Berlin, Vienna, Hamburg, Tel-Aviv, Düsseldorf, na Prague.

Safari ya kwanza itazinduliwa Jumanne, Desemba 13, 2016 na wasafiri wataondoka Istanbul saa 6:30 usiku na ndege TK567 itakayowasili saa 3:30 asubuhi. Watarudi na ndege hiyo TK567 itakayoondoka Zanzibar saa 4:25 asubuhi na kuwasili Istanbul saa 11:45 jioni.




Safari za Instanbul – Kilimanjaro – Zanzibar – Istanbul (IST-JRO-ZNZ-IST) zitakuwa tatu kwa wiki. Utaratibu wa kuweka mpango wa safari unapatikana kupitia tovuti www.turkishairlines.com kama ifuatavyo::

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...