Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Alhamisi ya tarehe 08 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.

Baaada ya mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.

Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuia ya Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.

"Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudani ya Kusini liwe Taifa lenye amani,hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu"

Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.

"Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo,ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudani ya Kusini"

Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam

08 Desemba, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Rebecca Nyandeng De Mabior mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mabior Garang Mtoto wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudani Kusini Hayati John Garang De Mabior Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...