MKAZI
wa kijiji cha Kabare kata ya Uwarama wilaya ya Kakonke, Robent Laurent
(35) ametoweka nyumbani kwake Dodoma Makulu katika mazingira ya
kutatanisha.
Kwa mujibu wa Shemeji yake, Mchungaji Philip Kayanda, amesema kuwa Laurent alikuwa ametokea Zanzibar na kuelekea Kahama lakini alipofika hapa Dodoma aliteremka na kuelekea nyumbani kwao eneo la Dodoma makulu ambako alitoweka kusikojulikana. Pia alisema kuwa shemeji yake huyo ana matatizo ya akili.
Laurent ambaye rangi yake ni maji ya kunde amesema kabla ya kujachanganyikiwa akili, alikuwa anafanya kazi ya uchungaji katika kanisa la FPCT huko kijijini kwao Kabare mkoa wa Kigoma ikiwemo na Zanzibar.
Amesema jitihada za kumtafuta kwa ndugu, jamaa na marafiki zimefanyika bila mafanikio na tayari wametoa taarifa kituo cha polisi kati cha Dodoma na kufungua jalada namba RB/DOM/8409/2016.
Ameomba kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa katika kituo chochote cha polisi kilichopo karibu ama apige simu namba 0688 - 688229,0788 – 669300 au 0655 – 090820

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...