Ndugu John Pombe Joseph Magufuli 

Alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke  na watoto saba.  Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora  za jamii na kero zao zinaondoka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2016

    Huyu ni Rais wetu na pamoja tunamuunga mkono. Tunahitaji awe na mamlaka zaidi ya kukiongoza Chama ChaMapinduzi. kisafike na kibaki na hisoria nzuri. Nenda baba nenda chukua chama na twende mbele. Hatutaki kurudi nyuma kwani safari uliyotuanzishia ni nzuri na wote tunafaidika. Mwenyezi Mungu awe nawe, awew naso sote na Taifa lote pia.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 23, 2016

    Raisi fiti. ila kuwatia moyo wanafunzi wa secondari ungeweka wazi divisheni na pointi ulizopata form IV na form VI na GPa ya BSC. We mwalimu tupe moyo tukuige kwa namba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...