Picha na Habari na Frank Mvungi-Dodoma
Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekabidhiwa ripoti ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Bungeni mjini Dodoma leo.
Akizungumza wakati akipokea Ripoti hiyo Naibu Spika amesema kuwa ripoti hiyo ni muhimu kwa Bunge na ni kiashiria cha ushirikiano mzuri kati ya Bunge na Tume hiyo.
“Ushirikiano uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mzuri na kwa upande wangu natumaini tutaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali,” alisisitiza Mhe. Dkt.Tulia.
Akizungumzia majukumu ya Bunge naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia amesema kuwa Bunge la kumi na moja limetimiza majukumu yake vyema  hali itakayochochea  maendeleo hapa nchini katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya tano      
Kwa upande wake mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva amepongeza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tume hiyo na Bunge kama mdau muhimu na kuahidi kuuendeleza kwa maslahi ya pande zote.
Ziara ya Tume hiyo pamoja na kukabidhi ripoti hiyo kwa Naibu Spika ililenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Tume hiyo kuhusu majukumu ya Bunge ambapo wajumbe hao walitembelea maeneo mbalimbali ya Bunge.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa  ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akikabidhi ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Bungeni Mjini Dodoma mara baada ya Kuirishwa kwa Bunge jana.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na ujumbe wake wakiangalia moja ya vitabu vilivyopo kwenye maktaba ya Bunge wakati wa Ziara yao Bungeni mjini Dodoma.
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ujumbe wake mara baada ya ziara ya Tume hiyo Bungeni Mjini Dodoma leo.kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva na kulia Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Hamid Mahamud Hamid.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva akiongoza ujumbe wa tume hiyo kwenye viwanja vya Bunge leo wakati wa Ziara ya kutembelea Bunge na kuwasilisha ripoti ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...