Mwanamuziki kutoka Jamhuri wa Demokrasi ya Congo Koffi Olomide amesafirishwa kwenda mjini kinshasa kutoka Nairobi baada ya kukamatwa Ijumaa usiku.

Olomide alisafirishwa na shirika la ndege la Kenya Airways, kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta mwendo wa saa tano unusu asubuhi.

Mwanamuziki huyo alikuwa amekabiliwa na shutuma baada ya kanda ya video kuenea mtandaoni ikionekana kumuonyesha akimshambulia mwanamke uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta Ijumaa asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili.

Mwanamke huyo anadaiwa kuwa mmoja wa wachezaji ngoma wake.

Akiongea katika kituo cha televisheni ya Citizen, muda mfupi kabla ya kukamatwa, Olomide alijitetea na kusema hakukusudia kumshambulia mwanamke huyo.


Alisema alikuwa ameingilia kisa ambacho aliamini ni mtu aliyetaka kumpokonya mmoja wa wachezaji densi wake pochi yake au kulikuwa na vurugu fulani.

Olomide alikamatwa muda mfupi baada ya kumaliza mahojiano katika kituo kimoja cha runinga jijini Nairobi.

Mkuu wa polisi nchini Kenya Joseph Boinnet alikuwa ametoa taarifa na kuwaagiza polisi wachukue hatua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2016

    Fukuza msukule huu, lazima tusimame pamoja kupinga unyanyasaji wa Wanamaker was namna hii

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 25, 2016

    koffi pamoja na kuishi kwake ulaya kwa muda mwingi lakini bado hajastarabika kupiga madansa ndio zake

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...