Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa Nasaha maalum mara baada ya kumaliza kufuturu na watoto Yatima kwenye viwanja vya Karimjee iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi television cha Mboni Show.
Mkuu wa Wilaya ya kinondoni Mhe. Ally Hapi (kushoto) akiwa kwenye dua pamoja na wageni waalikwa wengine.
Watoto Yatima wakiswali wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha televisheni cha Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kufanyika kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kushoto) akisalimiana na Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) mwingine pichani ni Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess inayotengeneza kipindi cha television cha Mboni Show Bi. Mboni Masimba wakati wa tafrija ya kufuturisha watoto yatima iliyofanyika kwenye viwanja vya Karimjee. 
Mkurugenzi wa kampuni ya Chocolate Princess kinachoandaa kipindi cha The Mboni Show akizungumza wakati wa kufuturisha watoto yatima .
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda akizungumza kwenye tafrija ya kufuturisha Watoto Yatima iliyoandaliwa na kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa na kipindi cha television Mboni Show ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan .(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Watoto wakipewa juisi wakati wa Tafrij ya Futari.
Naibu Mufti Mkuu Sheikh Hamid Jongo akizungumza kwenye tafrija hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuvisimamia kwa ukaribu vituo vyote vya kulelea watoto yatima nchini na vituo ambavyo vitabainika kuwa vinanufaisha wamiliki na vinaendeshwa bila ubora vitafungiwa mara moja. 

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Chocolate Princess inayoandaa kipindi cha Mboni Show hafla iliyojumuisha watoto yatima 283 kutoka Vituo vitano vya Mkoa wa Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa azma ya serikali ni kuona vituo vyote vya kulelea watoto yatima kote nchini vinatoa huduma bora na inayokidhi mahitaji ya watoto hao na sio vinginevyo. Kuhusu malezi ya Watoto yatima, Makamu wa Rais ametoa wito kwa jamii iendelee kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia elimu bora,upendo na si kuiachia serikali mzigo huo au mashirika yasiyo ya kiserikali. 

Aidha, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameiomba jamii kuweka mipango mizuri ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto yatima kwa kuwa nao wana haki ya kuishi vizuri kama watoto wengine. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...