Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akitoa hoja kwa Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma huku akishudiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo (hayupo pichani) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Dodoma)
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na mwalimu wake Maria Mnkumbo (katikati) aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma. Kushoto ni mke wa Waziri Mwigulu Neema.
Mwalimu msataafu Maria Mnkumbo aliyemfundisha Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida akiwa ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba akiwa na mwalimu wake Maria Mnkumbo aliyemfundisha darasa la kwanza na la pili katika shule ya msingi Makunda iliyopo wilaya ya Iramba Mkoani Singida mara baada ya waziri huyo kutoa hoja ya Bunge kuidhinisha makadirio na matumizi ya fedha ya wizara yake kwa mwaka 2016/2017 leo mjini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 04, 2016

    Kazi ya ualimu ni ya kujivunia sana matokeo ya kazi yao kwa taifa wanayaona haraka ni dhahiri siyo kama kazi zingine. Hongera mwalimu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 04, 2016

    Nimefurahishwa sana na waziri Mwingulu kwa kukumbuka tuliko toka na mchango wa waalimu wetu toka ngazi mbalimbali na ugumu wa mazingira wanayo pambana nayo ikiwa ni pamoja na manesi, madaktari na mapolisi.

    ReplyDelete
  3. Hongera na Pongezi za dhati Mh. Waziri Mwigulu Nchemba kwa kumkumbuka mwalimu wako na kwa heshma kubwa na taadhima ya kutoa hoja Bungeni, ili kutaka bajeti ya Wizara yako kuidhinisha makadirio na matumize ya fedha kwa mwaka 2016/2017 huku ikishuhudiwa na Mwalimu wako wa darasa la kwanza na la pili Bi Maria Mnkumbo. Ni fakhari iliyoje ya kumuenzi mwalimu wako, kitendo cha kushuhudia tu mwanafunzi wake au kupewa fursa hiyo na mwanafunzi wake ni jaza tosha katika kumuenzi Mwl. Bi Maria Mnkumbo. Naamini ombi la hoja yako litakubaliwa na kupokelewa kwa moyo mkunjufu kwa asilimia zote.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 05, 2016

    Hongera Mwalimu na Nakushukuru Waziri kumkumbuka mwalimu wako.Lakini muhimu wasaidieni hawa walimu wastaafu mafao yao ni madogo sana .Waziri nakuomba liangalie hili, walau wapate hela ya kuwakimu mahitaji yao yote maana wamefanya kazi nzuri walistahili kuishi vizuri katika uzee wao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 05, 2016

    Safi sana Mchemba! Mwalimu yuko na ule usiliasi wa ualimu kweli kweli. Ila hakikikisha unaingiza mkono mfukoni kabla hujaagana na ticha!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Mh. Waziri kwa kumkumbuka mwalimu. Inaonyesha ni kwa jinsi gani una upendo na unajali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...