Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema vita inayoendeshwa na Serikali ya awamu ya tano dhidi ya wala rushwa na wale wanaofanya ufisadi siyo nguvu ya soda kama wengi wanavyofikiri.

“Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kupambana na wala rushwa na mafisadi. Wala hatutanii. Hawa tutacheza nao na wala wasidhani vita hii ni nguvu ya soda. Tutaendelea kuwasaka hadi tufike mwisho,” alisema Waziri Mkuu wakati akizungumza na Watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika kwenye Ubalozi wa Tanzania jijini Lusaka, Zambia juzi jioni (Jumanne, Mei 24, 2016).

“Hatutaki tabia iliyokuwepo ya mwananchi anakuja ofisini kutaka huduma lakini hasikilizwi hadi atoe chochote, sisi hiyo tabia hatutaki kuisikia kabisa. Tumedhamiria kurudisha heshima kwenye utumishi wa umma na nimeanza kupata faraja kwani sasa hivi (nimeambiwa) katika baadhi ya taasisi unasikia mtu akiulizwa una shida gani, nenda pale, jambo ambalo zamani halikuwepo,” alisema.

Alisema Serikali imeamua kupigia debe dhana ya utumishi wenye uadilifu kwa sababu huo ni utamaduni mpya. “Ni kipindi kigumu kidogo cha mabadiliko lakini tumesimamia mabadiliko haya na ndiyo maana watumishi wote tumewasisitizia kuwa suala la uaminifu, uadilifu na uwajibikaji ni muhimu,” alisema na kuongeza.

“Hatutamvumilia mtumishi yeyote ambaye hatakuwa tayari kuwatumikia Watanzania au atakayeendekeza uzembe lakini pia hatutamuonea mtu yeyote. Hapa tunasisitiza usawa na hatutaki kutengeneza gap kati ya mwananchi mtumishi na wa mwananchi wa kawaida, tunataka kila mwananchi aione Tanzania ni nchi yake na kila kinachozalishwa ni sehemu yake. Tukifika hapo, tunaamini kila mmoja ataweza kuisemea nchi yake.” 

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2016

    Safi na hongera. Kweli mambo yameanza kubadilika.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2016

    Tukifanikiwa kuondoa rushwa tutafaidika kihuduma na kuweza kutumia mapato yetu kuongeza mapato ya wengi. Zipo nchi zilizofanikiwa zikiwemo za Afrika kuondoa rushwa. Mambo yote yanafanyika kwa utaratibu mzuri hakuna wa kulalia wengine kwa ajili ya kujinufaisha na mali ya umma.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2016

    Lakini kuna maeneo kama polisi kidogo kazi ipo. Serikali hii imefanya kazi kubwa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...