KIKOSI cha timu ya soka ya Tanzania – Taifa Stars, chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kinatarajiwa kuondoka kesho saa 12.00 alfajiri kwenda Nairobi, Kenya kucheza na Harambee Stars katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei 18, 2016 mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo unadumisha uhusiano na upendo wa enzi wa nchi za Kenya na Tanzania na umeingizwa kwenye orodha ya viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Kikosi cha Stars kina makipa, Deogratius Munishi (Young Africans), Aishi Manula (Azam FC) na Benny Kakolanya (Tanzania Prisons) wakati mabeki ni Mwinyi Haji na Juma Abdul (Young Africans), Aggrey Moris, David Mwantika na Erasto Nyoni (Azam FC), Mohammed Hussein (Simba) na Vicent Andrew (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao, Farid Mussa (Azam), Jonas Mkude na Mwinyi Kazimoto (Simba), Mohammed Ibrahim na Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar), Ismail Issa (JKT Ruvu), Juma Mahadhi (Coastal Union) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), Mbwana Samatta (KDC Genk), Elias Maguli (Stand United), Ibrahim Ajib (Simba), John Bocco (Azam), Deus Kaseke (Young Africans) na Jeremiah Juma (Tanzania Prisons).

Wakati huohuo.
SERENGETI BOYS.
TIMU ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inatarajia kutua leo Mei 26, 2016 saa 1.15 jioni baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kimataifailiyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Serengeti Boys haikuwahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano hiyo baada ya kutoka sare mechi tatu na kushinda mmoja kabla ya kuingia hatua ya kucheza mshindi wa tatu ambako ilishinda mabao 3-0 jana dhidi ya Malaysia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...