MADEREVA wa magari waaswa kuwa makini wakati wakiendesha magari hasa katika makutano ya magari ya mwendo wa haraka yanayotoa huduma za usafari jijini Dares Salaam.


Hayo yamesikika na shuhuda mmoja wakati wa ajali iliyotokea katika makutano ya Barabara ya BRT na Bibititi Mohamed eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 5 katika eneo la Chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC na gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.




Ajali imetokea katika makutano ya barabara ya Bibititi Mohamed na barabara ya BRT  maeneo ya  chuo cha CBE  jijini Dar es Salaam ikiwa ajari hiyo imetokea kati ya Gari lenye namba za usajili T 713 DFC lililokuwa likitokea Mnazi mmoja kuelekea Maktaba na kugonga gari la mwendo wa haraka lililokuwa likitokea Kivukoni.
Chanzo cha ajali hiyo ni Mataa ya makutano ya barabara hiyo kutokufanya kazi ya kuongoza magari.

 Gari lenye namba za usajili T 713 DFC  likiwa limeharibika mara baada ya kugonga gari la Mwendo wa haraka katika eneo la chuo cha CBE jijini Dar es Salaam leo.
 Gari lenye namba za usajili T 713 DFC ambalo limeharibika kwa kugonga gari la mwendo wa haraka likivutwa na Breakdown kuondolewa eneo palipokuwa na ajali hiyo eneo  chuo cha CBE na katika makutano ya barabara ya BRT na Bibititi Mohamed jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2016

    Nafikiri watu wanakosa tu umakini barabarani hasa junctions, halafu hawatakiwi kutumia barabara za hayo mabasi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2016

    Alama za stop kama hazipo ziwekwe ni mapema kuwa na ajali kama hizi wahusika washirikiane na trafiki kushughulikia hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...