Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye aanza ziara ya kutembelea  vituo, pamoja na kujitambulisha kwa maafisa na askari kwa mara ya kwanza kwa kuanzia  mkoa wa dar es salaam.

Katika ziara hiyo Kamishna Jenerali alipata fursa ya kukagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula liliopo mkoa wa kinondoni kwa ajili ya kurahisisha upatikani wa huduma kwa askari.

Pia amesisitiza kufufua visima vya maji ya kuzima moto (fire hydrant) kwa kushirikiana na ofisi ya idara ya maji  ili kurahisisha kupatikana kwa maji yanapohitajika na jeshi la zimamoto na uokoaji.

Amesema kuwa kwa kushirikiana nao itasaidia kufufua visima vilivyokufa au kuingiliwa na makazi ya wananchi na kufanya zoezi la upatikanaji wa  maji ya  kuzima moto kuwa karibu na  wazimamoto watapata maji na kurudi kwenye tukio kwa haraka zaidi.
Konstebo Said Sengendu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kituo cha Ilala akitoa maelezo ya utumiaji wa vifaa mbalimbali vilivyopo katika magari ya kuzima moto na maokozi kwa Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo,  Thobias Andengenye . (Picha na FC Godfrey Peter)
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (wa kwanza kushoto) akiongozwa na Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Msaidi Peter Mabusi wakikagua mradi wa ujenzi wa bwalo la chakula lililopo katika kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Lugalo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye (aliyeketi kulia) akipokea taarifa ya utendaji kazi kutoka kwa Kamanda Kanda Maalumu ya Dar es salaam, Kamishna Msaidi, Jesuald Ikonko alipotembelea kituoni hapa leo hii mapema asubuhi katika ziara ya kutembelea vituo vya zimamoto nchini.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akipokea maelezo kutoka chumba cha mawasiliano namna ya upokeaji taarifa ya miito ya dharura .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 05, 2016


    Kunradhi,
    Nitasema si-kizalendo lakini kuna ukweli.
    Nchi hii ina majeshi mesngi mno. kwa nini pasiwepo jeshi moja ambalo ndo lina wataalamu tofauti? Kwa mfano, kwa nini JW, Polisi, Magereza zote zina hospitali zao na waganga wao tofauti. JW, Polisi zote zina vikosi vya zimamoto tofauti na Jeshi la zimamoto. JW, Polisi, Uhamiaji, vyote vina wanamaji. Hii hufanya kutawanya utaalamu na kuondoa ushirikiano ambao ungejenga ujuzi mkubwa utokanao na uzoefu wa ushirikiano. Pia gharama za mafunzo na uendeshaji vikosi vifanyavyo kazi moja bila ushirikiano. Nchi masikini na ni sababu ya mipango na miundo ya kimasikini ambayo itafanya umasikini zaidi. Mduara wa umasikini endelevu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...