Katibu Mkuu wa baraza la michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja.

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BARAZA la Michezo (BMT) limealaani kitendo cha Muandaaji  Ngumi za kulipwa  (PST) Emmanuel Mlundwa kwa kitendo cha Kuwachezesha vijana wadogo wenye umri wa kati ya miaka 7-8 katika pambano la kimataifa lililofanyika Me 21 Jijini Dar es salam na tayari wameshamuandikia barua ya kutaka kujieleza kwanini wasichukuliwe hatua.

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja amesema wamempa siku saba kuanzia jana na wanataka ajieleze kwanini amewachezesha watoto hao ikiwa serikali inapinga ajira kwa watoto na hawawezi kuona hilo linafanyika tena ukilinganisha kuwa katika kanuni za mchezo wa ngumi hazijaweka sheria kwa watoto wadogo kucheza huku wakiwa wanacheza nyakati za usiku na kitu ambacho hakizuruhisiwi kabisa.

"PST wamefanya kitu ambacho hakiruhusiwi kabisa kwenye suala la kuwachezesha watoto wa wadogo tena usiku na wanafahamu kuwa sheria za haki za watoto hawaruhusu watoto wadogo kufanya kazi ambazo haziruhusiwi pia tunataka watupe majibu yao ndani ya siku saba,"amesema Kiganja.

Wakati huo huo.
UMISETA TAIFA KUFANYIKA KANDA YA ZIWA MWAKA HUU, KUANZA JUNI 13.
Kiganja amesema kuwa kwa mwaka huu Mashindano ya UMISETA yanatarajiwa kufanyika Jijini Mwanza kuanzia Juni 13 hadi 26 na kuzinduliwa katika viwanja vya CCM kirumba huku shule zikiw tayari zikmeshajindaa kuweza kuibua vipaji vipya kwani wanamichezo wengi ikiwemo wa Riadha,mpira wa miguu na pete wametoka katika michezo mashuleni.

"Umiseta mwaka huu inatarajiwa kuwa ya aina yake na shule zimeonekana kujiandaa kuweza kupata na kuibua vipaji vipya kwa vijana wadogo, pia mashindano haya yanafanyika Jijini Mwanza kwani tumeonelea kupeleka kanda ya ziwa kwani tunataraji kupita kanda zote nchinj na malengo makuu ni kurudisha michezo mashuleni,"amesema Kiganja.

Mashindano haya yatakuwa ni kwa nchi nzima ikiwemo mikoa ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar na hii itakuwa ni mwanzo mzuri wa kurejesha michezo mashuleni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...