1.MTUNGI WA MAJI(WATER)
Mtungi huu una rangi NYEKUNDU wote. Mtungi huu hautumiki kuzimia moto wa umeme au mafuta, ila unazima aina nyingine zote za moto. Mtungi huu ni hatari sana kuutumia kwenye moto wa umeme

2. MTUNGI WA KABONDAYOKSAIDI(CO2)
Mtungi huu hutumika kuzima aina nyingi za moto ukiwamo umeme. Ni mwekundu lakini una lebo NYEUSI kama kitambulisho chake. Wakati wa kuzima moto usishike mwishoni mwa bomba kwakuwa gesi inayotoka ni ya baridi sana unaweza kuganda. 3. MTUNGI WA POVU(FOAM) Mtungi huu una rangi ya KRIMU kama kitambulisho chake. kwingine kote ni mwekundu. Unazima moto wa vitu vya majimaji pamoja na vitu vigumu 4. MTUNGI WA PODA(POWDER) Mtungi huu una lebo ya BLUU kama kitambulisho chake. Unaweza kuzima moto wa gesi, majimaji, na vitu vigumu.


5. MTUNGI WA DAWA/KEMIKALI(Chemical)
Mtungi huu una lebo ya NJANO kama kitambulisho chake. Unazima aina nyingi za moto ukiwamo wa mafuta.
KUMBUKA: Mtungi wa kuzimia moto si kwaajili ya kuufanya moto usiendelee kuwaka bali kukufanya upate njia ya kujiokole hasa ukiwa ndani ya nyumba yako. Kwa udogo wa ule mtungi huwezi kuzima moto unaunguza nyumba nzima. Kama moto umezuia mlango, chukua mtungi elekeza pale mlangoni ili moto uzimike upate kwa kutokea
Unapozima elekeza bomba la tingisha chini ulipo mot sio juu ya moto.

Imeandaliwa na RSA na Dj sek Blog


Mitungi ya zimamoto hutofautishwa kutokana na lebo za rangi zake (codes). Mfano Dry powder-Bluu; Kabondayoksaidi-Nyeusi. Na kila mmoja una kazi maalumu tofauti na mwingine. Penginepo hutumia herufi A,B,C


Herufi A ni kwa mtungi unaozima moto wa karatasi,mbao, plastiki,nguo,mipira na takataka
Herufi B ni kwa mtungi unaozima moto wa gesi,mafuta, rangi na solventi
Herufi C ni kwa mtungi unaozima moto wa nishati kama umeme na mafuta.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Baada ya kununua Mtungi kuelimishwa jinsi kuzima moto gharama nishingapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...