Wafanyakazi wa Airtel wakifanya ukarabati bucha la kijana Hashim Mikidadi, kijana aliyewezeshwa na Airtel kupitia mpango wake wa Airtel fursa Tunakuwezesha, wakiongozwa na Asisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (katikati) Mwishoni mwa wiki .Hashim ni kijana mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro. 
 Afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita, akikarabati duka la kijana Hashim Mikidadi mkazi wa Ngerengere mjini Morogoro aliyewezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa. Wafanyakazi wa Airtel walijitokeza kumsaidia kijana Hashim,  mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake  lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro baada ya kubahatika kuwezeshwa na mpango huo wa Airtel Fursa kwa kupatiwa vitendea kazi mbali mbali na elimu ya mafuzo ya biashara ya ujasiriamali.
Afisa mauzo wa Airtel Aminata Keita (kushoto) akiongea na kijana Hashim  mkazi wa Ngerengere mjini Morogoro aliyewezeshwa na Airtel Kupitia mpango wake wa Airtel Fursa walipoungana nae katika ukarabati wa bucha lake kabla ya kukabidhiwa vitendea kazi mwanzoni mwa wiki ijayo.

Katika jitihada za kusaidia vijana wajasiriamali, wafanyakazi wa  Airtel wameungana na shirika lao kupitia mpango wake wa Airtel FURSA kuwafikia vijana mkoani Morogoro. Mwishoni mwa wiki hii wafanyakazi hao walijitokeza kumsaidia kijana Hashim Mikidadi, kijana mjasiriamali  anayejihusisha na kuuza bucha la nyama kwa kukarabati duka lake  lililopo standi ya mabasi Ngerengere mjini Morogoro..

Akizungumza wakati wa zoezi la ukarabati wa bucha hilo Afisa mauzo wa Airtel, Aminata Keita alisema "Airtel tunajali sana jamii yetu inayotuzunguka hivyo tunaelewa changamoto nyingi ambazo vijana wamekuwa wakikutana nazo ikiwa ni pamoja na ukosefu wa ajira, ukosefu wa mtaji wa kuanzisha biashara zao na mambo mengine mengi. Msaada wetu kama wafanyakazi wa Airtel ni kuunga mkono mpango wa kampuni yetu ya kusaidia vijana hapa nchini ujulikanao kama Airtel Fursa  katika kusaidia vijana wetu kwa kuwaonyesha njia ili waweze kuinua jamii inayowazunguka na kufikia ndoto zao."

"Leo tunafuraha kubwa kuona kwamba tumeweza kumfikia na kumuwezesha kijana huyu mjasiriamali aliyewezeshwa na Airtel FURSA, ambaye Airtel Fursa imebadilisha maisha yake kwa kukarabati paa la bucha lake, kutengeneza sakafu kwa kuweka tiles za kisasa, na matengenezo mengine mengi ambayo imeipa duka hilo mtazamo mpya kabisa . Mapema wiki ijayo Airtel FURSA itamalizia kwa kumuwekea vifaa vya kisasa  kabisa  vikiwemo vifaa vya  kukatia nyama, jokofu la kisasa la kuhifadhia nyama na vifaa vingine vnavyohitajika kwa kazi za bucha. Vifaa hivyo na gharama za utengenezaji vimegharimu kiasi cha sh. milioni 9, alisisitiza Aminata

Wakati wa shughuli hiyo ya makabidhiano, wafanyakazi wa Airtel walijiunga na wakazi wa  Ngerengere ambao walijitokeza kumuunga mkono  Hashim kwa kuwa na nidhamu kwa jamii inayomzunguka na ni mfano wa kuigwa na vijana wenzie.

Kwa upande wake Hashim aliwashukuru sana Airtel kwa kuweza kumpatia  fursa hii kwani ni vijana wengi sana wanaohitaji msaada huu lakini leo hii nafasi hii imemdondokea yeye.“Bila kuwasahau nawashukuru sana wafanyakazi wa Airtel kwa kusaidia ukarabati wa bucha langu kwani mtazamo huu mpya  na vifaa vya kisasa utasaidia kuhamasisha wateja wangu na wale ambao hawakuwa wateja wangu.”.

“Nilianza nikiwa sina kitu. Lakini leo Airtel imeinua maisha yangu na kuniwezesha kuwapatia ajira vijana wenzangu waliokuwa mtaani bila kazi. ".
Airtel Fursa uwezeshaji ilizinduliwa mwezi Mei mwaka jana na ina tarehe kufikiwa vijana zaidi ya 3000 na mafunzo ya ujasiriamali na misaada ya biashara kwa karibu na 100 wajasiriamali bora vijana wote mmoja mmoja na katika vikundi vya vijana na hatimaye kukua kujenga fursa na jamii inayowazunguka. Katika msimu wa pili Airtel imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 katika mpango wa kuwawezesha vijana wa Tanzania kufikia uwezo wao katika ulimwengu wa biashara

Airtel Fursa awamu ya kwanza ulianza mwaka jana mwezi wa tano na mpaka sasa umeshaweza kufikia vijana zaidi ya 3000 kwa kuwapatia mafunzo ya biashara ya ujasiriamali na wengine wapatao 100 wameweza kuwezeshwa kwa kupatiwa vitendea kazi vya kuendelezea biashara zao za ujasiriamali. Katika awamu ya pili Airtel Fursa imeahidi kutumia zaidi ya sh. bilioni 1 ukiwa na lengo la kuwawezesha vijana kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za biashara na vifaa vitakavyowawezesha kukuza biashara zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...