Watu zaidi ya elfu 3 mkoani Morogoro hawana mahali pa kuishi baada ya kukumbwa na mafuriko kutokana mvua kubwa zinazonyesha. https://youtu.be/ic2oVMB3O9I

Rais John Mafuguli atoa jibu la mkwamo wa kisiasa visiwani Zanzibar huku akivitaka vyama vya upinzani vilivyosusia uchaguzi wa marudio kubadili maamuzi yao na kushiriki uchaguzi huo.https://youtu.be/6qu3UUvr1FU

Serikali yaanza kutoa semina elekezi kwa maafisa watendaji wakuu wa serikali, maafisa waandamizi wa serikali kuu na serikali za mikoa na maafisa wa juu wa jeshi juu ya umuhimu wa usalama wa taifa na uzalendo. https://youtu.be/_CwAyYtAi2M

Mpango wa taifa wa damu salama nchini wazindua kituo kidogo cha uchangiaji damu salama kilichopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es salaam. https://youtu.be/5S_GePdQI0w

Mawaziri wa zamani Basil Mramba na Daniel Yona waanza kutumikia kifungo cha nje kwa kufanya usafi katika hospitali ya  Sinza Palestina kwa kukabidhiwa vifaa vya usafi. https://youtu.be/-MuytyZ3LmI

Rais John Magufuli atimiza ahadi ya kuipatia wizara ya katiba na sheria fedha kiasi cha zaidi ya bilioni kumi na mbili;https://youtu.be/_-3u9O7rDKI

Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi yafanya uteuzi  upya za nafasi mbalimbali za uongozi zilizowazi katika ngazi ya mkoa na wilaya;https://youtu.be/rNB-G4VQKwY

Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo amuagiza wakala wa umeme vijini REA kuhakikisha wasambazaji wazawa wanaosambaza umeme vijijini wanapewa kipaumbele;https://youtu.be/_QS5oagrgyc

Mahakama ya ardhi mkoani Arusha yaagizwa kushughulikia kesi za migogoro ya ardhi kwa wakati; https://youtu.be/H0J4OW27F0E


Serikali yawataka mabalozi na wawakilishi wa kimataifa waliopo nchini kufuata sheria na taratibu za nchi;https://youtu.be/mQIofKGEjTM

Wakala wa vipimo nchini WMA yasema inazidai kampuni zaidi ya 15 shilingi bilioni 4 kama ada ya kupimiwa mafuta;https://youtu.be/sctbO9x3g5s

Inaelezwa kuwa kasi ya mfumko wa bei  wa taifa kwa mwezi januari mwaka huu yashuka kwa asilimia 0.3;https://youtu.be/kco7st5AZAk


Wachezaji wa soka nchini washauriwa kuzingatia suala la nidhamu ili kuweza kufikia malengo yao; https://youtu.be/NiTAOuJ-XNE

Jeshi la polisi mkoani Ruvuma linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kuuza tiketi feki katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara baina ya Maji maji FC na Mgambo JKT;https://youtu.be/SSwo8eJZ9T4


Timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yatwaa kombe la CHAN baada ya kuitandika timu ya taifa ya mali kwa jumla ya goli 3-0; https://youtu.be/0wUtd3-senI

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohammed Shein atoa wito kwa mahakama visiwani humo kutoa haki kwa wakati;https://youtu.be/5uPUXhhqUmU

Inaelezwa kuwa wazee viswani Zanzibar wanakabiliwa na changamoto ya huduma ya usafiri; https://youtu.be/ukzg7jjj4AQ
Wananchi  wa vijiji vya Makunduchi visiwani Zanzibar washauriwa kujitokeza kwa wingi kupima afya  bure kupitia wataalam wa afya wanaokwenda kuwatembelea; https://youtu.be/Q0cJ4QGEiXY

Waliokuwa mawaziri waastafu wa serikali ya awamu ya tatu, Basil Mramba pamoja Daniel Yona waanza kutumikia adhabu ya kifungo cha nje kwa kufanya usafi  katika maeneo ya kijamii;https://youtu.be/hsXrvLUMUMc

Kaya zaidi ya 20 wilayani Uyui mkoani Tabora hazina makazi kutokana na nyumba zao kubomoka kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo; https://youtu.be/_e4xTb8jlSk  

Inaelezwa kuwa takwimu za kina zinahitajika katika kupambana na kukomesha suala la ukeketaji nchini; https://youtu.be/0-MZbOs2ADw

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...