LUTENI KANALI MARTIN J MSHAMI(RTD)

Leo umetimiza miezi sita na siku tatu,tokea ututoke katika dunia hii na kutuachia huzuni kubwa.Ikiwa leo ni siku ya kumbukumbu yako ya kuzaliwa tunajawa na huzuni kwa kuwa haupo nasi kusheherekea hii siku yako, lakini tunafarijika kwa kuwa umetuachia malezi mema yenye upendo na miongozo iliyo mema katika maisha.
Unakumbukwa sana na wanao Denis,James,Janet,Mary na Husna.Unakumbukwa pia na wajukuu zako Hellen,Caren na Methodius pamoja na kaka zako Francis,Michael na Paul,wadogo zako Richard,William,Augustino,Victor na Peter pamoja na dada zako Kighenda,Pauline na Mariana,mama wakubwa Hidaya na Mariam.

Unakumbukwa pia na jumuiya ya marubani Tanzania,wanajumuiya wa ndege za serikali na makamanda wenzako wa JWTZ,wana kikosi wa 603KJ Airwing na Air Defence Command.
Tunajawa na huzuni katika hali ya kibinadamu lakini tuna imani kuwa Mwenyezi Mungu amekupokea katika ufalme wake.
Tutakukumbuka daima baba yetu, 
Mwenyezi Mungu akupe pumziko la amani.

'Roho za wenye haki zi mikononi mwa Mungu wala mateso ya kifo hayatawagusa'(Hekima ya Sulemani 3:1)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...