Washiriki wa mchezo wa kukuna nazi wakishindana katika Bonanza la michezo ya Jimbo la Tunguu yaliyofanyika kiwanja cha Bungi Mkoa wa Kusini Unguja.
 Mmoja wa washiriki akifurahia kumaliza kukuna nazi.
 Mshiriki wa mbio za Baskeli Zainab Juma akimaliza mbio hizo akishikilia nafasi ya nne.
 Mgombea uwakilishi Jimbo la Tunguu kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM Simai Mohommed Said akiteta kitu na Mwenyekiti wa CCM Jimbo Tunguu Khatib Ramadhan Iddi (katikati) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali.
 Mwenyekiti wa CCM Jimbo Tunguu Khatib Ramadhan Iddi akizungumza na washiriki wa CCM Bonanza lililofanyika Bungi Mkoa wa kusini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ramadhan Abdallah Ali akimpa zawadi kepte wa tim ya Nage ya Bungi (B) Shida Saidi. (Kulia) mgombea Upunge wa Jimbo la Tunguu Khalifa Salim Suleiman. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mshindi wa kukuna nazi hapo anaeshangilia kama 'umesukuwa' haihesabiki, kwa kweli nimefurahi kusikia hili neno au huu mchezo wa 'nage' na kuona kumbe bado ungalipo, tena kwa timu maalumu khasaaaa! Nadhani pangechapuka zaidi na kuleta burdani asilia pangechezwa na Kobole, Hadimfundo, Kinyuki Kipenyapenya n.k. maana yote ina ushindani katika kuburudisha. By the way inaleta raha na khamasa, mbali ya kuwajumuisha pamoja wanajamii katika shughuli kama hizi za michezo, khususan kwa kufanya mabonanza mbali mbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...