Tatizo la watoto wa kike mkoani Mtwara kukatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali limepungua kwa kiasi kikubwa baada ya uwepo wa mradi wa “Hakuna wasichoweza” unaoendeshwa na T-Marc kwa ufadhili wa Vodacom Foundation. 
 Mradi huo umeonyesha mwelekeo wa kuweza kutatua matatizo yanayowakabili watoto wa kike kutotimiza wajibu wao wa masomo mashuleni, ikiwa ni pamoja na kutotimiza ndoto zao sambamba na kupunguza utoro. 
 Akizungumza wakati wakati wa mrejesho wa mwenendo wa mradi huo kwa wadau wa elimu wa mkoa huu, Meneja wa Mradi huo, Doris Chalambo alisema mradi huo ulioanza kutekelezwa mwaka 2013 kwa mkoa wa Mtwara ulilenga kufikia wanafunzi 10,200 wa shule za msingi kuwapatia elimu ya afya, namna ya kujisitiri wakati wa hedhi na kupatiwa vifaa vya kujisitiri ambapo katika thamini yake iliyotolewa chini ya utekelezaji wake kwa mkoa wa Mtwara umeonyesha kuwa na mafanikio makubwa baada ya kuweza kupunguza tatizo la utoro. 
 “Lengo la mradi ni kufikia wasichana 10,200 kwa mkoa wa Lindi na Mtwara lakini kwa mkoa wa Mtwara wanafunzi wapatao 7,077 tayari wamefikiwa na tumekuwa tukiwapatia elimu juu ya hedhi, elimu itakayomsaidia pindi anapokuwa kwenye hedhi afanye kitu gani pamoja na elimu ya afya na madhara ya mimba za utotoni sambamba na kumsaidia vifaa vya kujisitiri (pedi) na hii ni kutokana na kuwa suala la hedhi halizungumziwi kabisa katika jamii yetu hivyo mtoto anapata changamoto na kumpelekea kukosa shule kati ya siku 2 hadi tano ndani ya mwezi mmoja na kumrudisha nyuma kieleimu,”alisema Chalambo. 
 Aidha alisema changamoto wanazokumbana nazo katika kutekeleza mradi huo ni pamoja na baadhi ya shule kukosa miundombinu kama vyoo na chumba maalumu kwaajili ya kusaidia wasichana katika masuala ya afya na kuwa, Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili itakuwa mkoa wa Lindi. 
 “Katika kutekeleza mradi huu hatuwezi kufanikiwa bila ya miundombinu, tumegundua shule nyingi vyoo sio vizuri, kwahiyo bila kuendana na miundombinu sahihi hatuwezi kufanikiwa,”alisema Chalambo. Akizungumza kwa niaba ya katibu tawala mkoa wa Mtwara, Jose Kitenana alisema mradi huo umeweza kuleta mabadiliko katika mkoa huo na kuwa serikali imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha miundombinu ya shule inakuwa rafiki. 
 “Mpango huu ni mzuri na kwa sisi serikali hatuwezi kufanya kila jambo, hivyo kuna wadau tunashirikiana nao kama T-Marc kutoa elimu ya afya kwa wanafunzi kwa udhamini wa Vodacom Foundation ili kusaidia watoto wetu wa kike, na suala la miundombinu bado zipo taratibu ambazo zinafanyika kuhakikisha wanajengewa mazingira rafiki,”alisema Kitenana 
 Naye Mkuu wa Vodacom Foudation, Renatus Rwehikiza alisema wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa wanatekeleza mradi wa hakuna wasichoweza kwa lengo la kuongeza mahudhurio ya watoto shuleni na kuwa itapunguza kasi ya magonjwa,utoro na mimba za utotoni. 
 “Vodacom Foundation inatoa misaada kwenye jamii katika vipengele tofauti na sasa hivi tuna mradi wa ‘hakuna wasichoweza’ umegharimu kiasi cha 480 milioni ambao umetekelezwa kwa awamu na sasa kwa mkoa wa Mtwara tumefikia ukingoni tunasubiri kupata tathmini ya huu mradi na awamu ya pili tutakuwa mkoa wa Lindi lakini nina imani kwa kiasi kikubwa utasaidia kupunguza ile kasi ya utoro na mimba za utotoni na kumwezesha mototo wa kike kutimiza ndoto zake,”alisema Rwehikiza 
 Akizungumza mwanafunzi, Doreen Mvungi alisema mradi huo umeweza kuwapa maarifa namna ya kukabiliana na changamoto walizokuwa wakizipata pindi wanapopatwa na hedhi shuleni na kuondokana na aibu ya kuzomewa waliyokuwa wakiipata toka kwa wavulana. 
 “Najivunia kuwa sehemu ya walionufaika na Mradi huu ni mkombozi umetupa elimu ya afya, elimu namna ya kujisitiri tunapokuwa katika hedhi na imewasaidia wengi kwani siku hizi hamna tena ile zomea zomea na hata mahudhurio ya darasani yameanza kuwa mazuri kwa sisi wasichana tofauti na zamani msichana alipokuwa akipatwa na ile hali anashindwa kujua nini cha kufanya,”alisema Doreen
Baadhi ya wadau wa elimu wa Mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye warsha maalumu ya mrejesho  wa mradi wa”Hakuna wasichoweza” unaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi  Chuno ya Mkoani Mtwara,wakiendelea na masomo yao baada ya kunufaika na mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi ili waendelee na masomo yao mashuleni.Mradi huo umedhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.
Meneja Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark Tanzania Doris Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao ulikuwaunaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania. 
Meneja Mradi wa”Hakuna Wasichoweza” wa asasi ya T-Mark Tanzania Doris Chalambo,akitoa tathmni ya mrejesho wa mradi huo kwa wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Mtwara baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao ulikuwaunaowapa elimu ya hedhi na vifaa vya kustiwri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Foundation na kuendeshwa na T-Mark Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...