Mzee Simon Kamillius Membe wa Rondo, Mkoani Lindi, amefariki jana tarehe 3 Oktoba 2015 huko Mumbai, India alipokwenda kwa ajili ya matibabu.

Mipango ya mazishi inafanywa Dar es Salaam  nyumbani kwa mdogo wake Mhe Bernard Membe (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili nchini siku ya jumatatu mchana tarehe 5 Oktoba 2015 saa 9 alasiri.

Ibada na heshima za mwisho ‎kwa Dar es Salaam zitafanyika siku ya jumanne tarehe 6 Oktoba 2015. Mahala na muda wa tukio hilo utatangazwa hapo baadaye.

Mwili wa Marehemu utasafirishwa kutokea Dar es salaam kuelekea Lindi siku ya jumanne baada ya ibada kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Rondo, Lindi siku ya jumatano tarehe 7 Oktoba 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...