Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.
Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao.
Baadhi ya Wasanii wa Filamu nchini, wakimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya picha ya kuchorwa ya Mama.picha na Freddy Maro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...