Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd ya kutoka Marekani, Bw. Mayank Bhargava. Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Bhargava alimjulisha Balozi Mulamula kuwa kampuni hiyo imeshaanza kazi ya kufunga mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wa MW 5 kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Aidha, alitoa taarifa kuwa hivi karibuni kampuni hiyo itaanza mchakato wa kufunga umeme wa nishati ya jua wa MW 16 kwa ajili ya mkoa wa Shinyanga.

Bw. Bhargava akisisitiza jambo huku Balozi Mulamula akisikiliza kwa makini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Cyril Batalia ambaye ni Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd.

mazungumzo yakiendelea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...