Na Bashir Yakub.
Rufaa ni hatua ya kisheria ambayo hufikiwa na mhusika katika shauri fulani iwapo hakurushishwa na maamuzi. Rufaa sio mpaka uwe umeshindwa kabisa, hapana. Yawezekana ukawa umeshinda kesi lakini hukuridhishwa na kiwango ulichoshinda.Kwa mfano uliomba wavamizi waondoke katika nyumba yako na hapohapo wakulipe fidia. Mahakama ikatoa hukumu kuwa umeshinda wavamizi waondoke katika nyumba yako lakini ikasema wasikulipe fidia.
Mazingira kama haya unakuwa umeshinda lakini ukitaka unaweza kukata rufaa kulalamikia kutolipwa fidia. Kwa hoja hii tunaona kuwa kumbe kukata rufaa si lazima uwe umeshindwa badala yake unaweza kuwa umeshinda lakini ukawa hukuridhishwa na vitu fulani katika hukumu ambavyo unaweza kuvikatia rufaa ili navyo uvipate.
1.AINA ZA RUFAA KATIKA MASHAURI YA ARDHI.
Kisheria rufaa hutofautiana kutokana na aina ya mgogoro ulio mbele. Mgogoro wa kimkataba unazo namna zake na masharti yake katika rufaa, halikadhalika migogoro ya kudai fidia, migogoro ya kikazi, migogoro ya kifamilia na talaka, migogoro ya jinai, migogoro ya kibiashara n.k. Hii ina maana hata migogoro ya ardhi nayo inazo namna zake za rufaa. Katika mashauri ya ardhi mara nyingi migogoro huanzia baraza la ardhi la kata huenda mabaraza ya ardhi ya wilaya, mahakama kuu ya ardhi hadi mahakama ya rufaa.
Hizi zote ni mamlaka zinazoweza kuamua mashauri ya ardhi. Aidha aina za rufaa huweza kutokana na mpangilio huu kimahakama. Ipo rufaa inayotoka baraza la ardhi la kata kwenda baraza la ardhi la wilaya. Ipo rufaa kutoka baraza la ardhi la wilaya mpaka mahakama kuu ya ardhi. Na ipo itokayo mahakama kuu ya ardhi mpaka mahakama ya rufaa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...