Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akisaini kitabu cha maombolezi katika ofisi za Ubalozi mdogo wa India Zanzibar, kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa India, Avul Pakir Abdul Kalam kilichotokea Julai 27. (Picha na Salmin Said).

Na Khamis Haji (OMKR).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za rambi rambi kwa wananchi wa India kufuatia kifo cha mwanasayansi aliyewahi kuwa Rais wa nchi hiyo, Dk. Avul Pakir Abdul Kalam kilichotokea Jumatatu iliyopita.

Ametuma salamu hizo wakati alipozungumza na Balozi mdogo wa India hapa Zanzibar, Satendar Kumar huko katika ofisi za Ubalozi huo Migombani, ambapo Maalim Seif alifika kusaini kitabu cha maombolezi.

Maalim Seif amesema Kiongozi huyo ni msomi aliyetoa mchango mkubwa kwa Taifa la India hasa kutokana na mchango wake katika uvumbuzi wa vyombo vya anga za juu, kwa ajili ya matumizi ya kiraia na Kijeshi.

Maalim Seif amesema bila shaka kifo chake kimeacha pengo na masikitiko makubwa sio tu kwa wananchi wa India, bali kwa jamii ya wasomi Duniani, na amewataka wananchi wa India kuwa na subira katika wakati huu mgumu wa maombolezi. 

Abdulkalam (83) ambaye alipewa jina la umaarufu ‘mtu wa misaili wa India’ alishika nafasi ya Urais wa India mwaka 2002 kwa muda wa miaka mitano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...