KATIKA hali ya kukabiliana na changamoto nyingi kwenye sekta ya bodaboda, kampuni ya mawasiliano na matangazo ya Alternative Communication ya jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania na Jeshi la Polisi wametengeneza mfumo salama wa kumbukumbu kwa waendesha bodaboda ili kuwasaidia bodaboda na abiria wanaotumia usafiri huo kutambulika kwa urahisi inapotokea wamehusika katika matukio ya kihalifu.

Hatua hiyo inakuja kufuatia madai kuwa baadhi ya waendesha bodaboda wasiokuwa waaminifu hujihusisha katika matukio ya kihalifu au kutumiwa na wahalifu kuvunja Amani na kupotea bila ya kutambulika.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo Bw. Edward Mgaya amesema jijini Dar es Salaam kwamba tayari kampuni hiyo imekwisha wasajili boda boda 3,000 katika mfumo huo. Ameongeza kwamba wale waliosajiliwa pia watapata faida ya kupewa huduma ya bima, mafunzo ya usalama barabarani na Ujasiriamali.

Bw. Mgaya alisema wale wanaosajiliwa katika mfumo huo wanapewa koti (Reflectors) zilizo na namba ya usajili mbele na nyuma ya koti, Namba hiyo ni utambulisho kamili wa mwendesha pikipiki pia kwenye kofia zao (helmet) itabandikwa namba ya simu ya Kiongozi wa Chama cha Waendesha Boda boda husika.

“Mtu yoyote akiipiga namba ya chama cha waendesha boda boda na akataja namba ya usajili wa dereva wa bodaboda, mfumo utamtambua dereva huyo mara moja.

Bw. Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Boda boda wa Kanda ya Tabata, ameelezea kufurahishwa na utaratibu huo mpya wenye faida kubwa kwao, na kwamba mfumo huo utaboresha usalama katika eneo lake.
Mkurugenzi wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya Alternative Communication Bw. Edward Mgaya akizungumza na vyombo vya habari katika tukio la kuwakabidhi sare (Reflactors), waendesha boda boda zitakazosaidia kuwatambua katika mfumo maalum wa kompyuta. Mradi huu unaendeshwa na kampuni hiyo kwa ushirikiano na kampuni ya simu ya Vodacom na jeshi la polisi.
Bw. Ramia Mazwela, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Waendesha Boda boda wa Kanda ya Tabata, akizungumza na waandishi wa habari namna alivyoupokea kwa furaha utaratibu huo.
Waendesha boda boda wa Kanda ya Tabata wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa zoezi la kugawiwa sare (Reflactors) kwa ajili ya utambuzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...