Baadhi ya wanahabari  mkoa  wa Iringa  wakiwa katika picha  ya pamoja na viongozi  wa  jeshi la polisi mkoa wa Iringa mara baada ya  kumalizika  kikao  chao cha mahusiano mema na kutambulishana kati ya wanahabari na viongozi wapya wa  jeshi  la Polisi waliokaa ni kamanda wa polisi Ramadhan Mungi wa tatu  kushoto akifuatiwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard na katibu wa IPC Francis Godwin na maofisa wengine wa polisi mkoa.
 Na FG BLOG.
Wanahabari wa mkoa wa Iringa leo wamekutana na kamanda wa polisi na maofisa wa jeshi la polisi Mkoani hapa ili kuendelea kufanya Kazi kwa ushirikiano kwa faida ya Mkoa wa Iringa.

Katika kikao hicho kilichoambatana na semina fupi ya kukumbushana wajibu wa Kazi za wanahabari na askari.

Akitoa mafunzo hayo kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi amesema kuwa ili kuufanya Mkoa wa Iringa uweze kufanikiwa ni lazima wabahabari na polisi kufanya Kazi zao kwa kuzingatia maadili na kutofanya upendeleo katika utendaji wao.

Mungi alisema kuwa mbali ya kazi kubwa ambazo vyombo vya habari mkoani hapa vinafanywa bado jeshi lake limeamua kukutana na wanahabari hao ili kizidi kuufanya Mkoa kuwa na taswira nzuri ktk mahusiano Kati ya pande hizo mbili kama njia ya kuwatumikia wananchi.

Alisema kwa Mkoa wa Iringa vyombo vya habari vimeonyesha mchango mkubwa zaidi zaidi na kutaka mchango huo na jitihada hizo kuendelea zaidi .

Kamanda Mungi amesema kuna haja ya wanahabari na askari polisi kuendelea kujenga mahusiano kwa kukutana na viongozi wao kabla ya kufanya mapambano yasiyo na tija.

Alisema kuwa wao kama jeshi la polisi wanatambua kuwa vyombo vya habari ni muhimu kwa jamii hivyo lazima kujenga mahusiano mema na kuwa askari polisi hawanasababu ya kuendeleza mivutano 

Alisema kuwa kuna wakati mwingine ajali imetokea na Kazi ya mwanahabari ni kuhabarisha umma na polisi kuokoa hivyo lazima kufanya Kazi kwa karibu na kutoa majibu stahiki kwa wanahabari na wanahabari kutotumia jazba katika utendaji Kazi zao .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...