Na Othman Khamis Ame Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Watendaji wa Taasisi za Serikali wana wajibu wa kutumia vipaji walivyojaaliwa kuwa navyo katika kubuni mbinu na mikakati watakayohisi kwamba inaweza kutaleta faida na ufanisi katika maeneo yao ya kazi sambamba na Serikali  Kuu kwa jumla.

Alisema faida ya ubunifu watakaoutumia watendaji hao utaongeza kasi ya uwajibikaji endapo wataendelea kushikamana baina yao katika kufanya kazi kwa juhudi, maarifa na nidhamu kwa kutumia vipaji hivyo.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa hafla maalum ya chakula cha usiku alichowaandalia watendaji wa Taasisi zilizo chini ya Ofisi yake kufuatia kukamilisha  na hatimae kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo pamoja na kuagana baada ya kufanya kazi pamoja katika kipindi chote cha miaka mitano tokea mwaka 2010.

Hafla hiyo ya chakula cha usiku iliyofanyika katika Makaazi ya Balozi Seif Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar ilijumuisha pia baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi wakuu wa Serikali, wafanyakazi wa Baraza hilo wakiwemo wawakilishi wa taasisi tofauti za ndani na nje ya nchi wanaofanya kazi pamoja na watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Balozi Seif aliwapongeza watendaji wa taasisi zote zilizo chini ya Ofisi yake kwa kufanya kazi nzuri katika utekelezaji wa majukumu yao likiwemo pia suala  la kutengeneza Bajeti na hatimae kupita bila ya vikwazo katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea.
 Kikundi cha Muziki wa Morden Taarab cha Big Staa chenye mastakimu yake Ofisi ya Mkoa Mjini Amani kikitoa burdani kwenye tafrija ya kuwapongeza Viongozi na watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar baada ya kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo pamoja na kuagana kwa kukaribia kukamilika kwa kipindi cha miaka mitano.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi  aliyepo mwanzo kushoto akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Baraza la Wawakilishi inayosimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Serikali Kushoto yake Mh. Hamza Hassan Juma na Mjumbe wa Kamati hiyo Mh. Makame  Mshimba Mabrouk  kwenye tafrija ya kuwapongeza watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
 Seif wapili kutoka kushoto akijumuika pamoja na Viongozi na watendaji wa Ofisi yake kwenye tafrija aliyowaandalia baada ya kupita kwa Bajeti ya Wizara hiyo katika Kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea.
  Baadhi ya Watendaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wakijipatia mlo kwenye tafrija hiyo iliyofanyika katika Makazi ya Balozi Seif yaliyopo Mazizini nje kidogo ya M,ji wa Zanzibar.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuzungumza na Viongozi na watendaji wa Ofisi yake.
 Balozi Seif akitoa nasaha zake mara baada ya kuwaandalia chakula cha usiku Viongozi na Watenmdaji wa Taasisi zilizochini ya Ofisi yake kufuatia kupitishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo pamoja na kuagana baada ya kufanyakazi pamoja katika kipindi cya miaka mitano iliyopita.
 Balozi Seif kati kati akiwa pamoja na wake zake Mama Pili Seif Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi wakijumuika pamoja katika kusakata rumba kwenye tafrija ya kuwapongeza watendaji wa Ofisi yake hapo Nyumbani kwake Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...