NMB imeibuka mshindi wa kwanza na wa jumla katika makampuni ya biashara yanayojali zaidi jamii kwa kutoa sehemu kubwa ya faida yake kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika jamii ya kitanzania.

Ushindi huo umetokana na utafiti uliofanywa na Taasisi ya utafiti wa huduma za maendeleo ya jamii - Research Centre for Social Development Services kwa kushirikiana na kampuni mwenza ya konsalt limited imetoa tuzo hiyo kwa NMB baada ya kujiridhisha kuwa ndiyo benki inayoongoza kwa kusaidia jamii zaidi.

NMB imeyapiku makampuni na benki zingine 9. NMB hutoa asilimia moja kwaajili ya kuchangia maendeleo hususani madawati mashuleni, vifaa mahosipitalini, kutoa elimu ya masuala ya fedha pamoja na kuchangia jamii kipindi cha majanga kwa kuchangia vifaa mbalimbali kwa wahanga.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Mtarajiwa wa NMB Bi. Ineke Bussermaker alisema “NMB imedhamiria mchango kwa jamii sio tu katika huduma za kibenki kwa wateja bali pia kutoa sehemu ya mafanikio yetu ili kuisadia jamii katika maeneo makuu matatu - kutoa elimu kuhusu huduma za kifedha, kuchangia katika sekta ya Afya, misaada mashuleni na mchango kwenye matukio ya maafa”.
 Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB-Bi Ineke Bussermaker akipokea tuzo ya Mshindi wa jumla kama taasisi inayochangia zaidi huduma za jamii kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Biashara -Abdala Kigoda.
Afisa Mtendaji Mkuu Mtarajiwa wa NMB - Bi Ineke Bussermaker pamoja na Waziri wa Viwanda-Abdala Kigoda wakipata picha baada ya makabidhiano ya tuzo hiyo.  

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...