Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteua Balozi Rajabu Hassan Gamaha kuwa Balozi wa Tanzania nchini Burundi.

 Balozi Gamaha anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Mwasi Nzagi ambaye amestaafu kwa mujibu wa sheria.
 Kabla ya uteuzi huo Balozi Gamaha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Uteuzi huo unaanza mara moja.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

27 Aprili 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Burundi kimewaka anakwenda kufanya nini....avute subira kwanza...

    ReplyDelete
  2. Hongera Balozi Ghamaha, kwa shughuli za kidiplomasia na kibalozi huu ndiyo muda anatakiwa kuwepo kituoni. Na kuishauri vizuri serikali kuhusu mahusiano baina ya nchi hizi mbili.

    ReplyDelete
  3. Kwani ubalozi kuna kustaafu kwa mujibu wa sheria?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...