Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya namna uzalishaji unavyofanyika kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Bellaview Fresh Fruits Processing Industry Ndugu Shanel John Ngowi.Kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuvuta waya wa umeme kwenye mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Kirongo Samanga ikiwa sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifungua maji ikiwa sehemu ya uzinduzi wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji cha Kahe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Lembris Marangushi Kipuyo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha ndoo ya maji Bi. Petronila Jakob kama ishara ya uzinduzi rasmi wa huduma ya maji katika kijiji cha Kahe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Tarakea wilayani Rombo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Tarakea Polisi.

Katibu Mkuu wa CCM anaendelea na ziara za kujenga na kuimarisha Chama mkoani Kilimanjaro pamoja na kukagua, kuhimiza utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010. Katika ziara yake ya leo wilayani Rombo ,Katibu Mkuu alishiriki shughuli mbali mbali ,zikiwemo kufungua ofisi ya chama ya wilaya, kukabidhi Bima ya afya kwa vijana 900 wa boda boda,Kukabidhi mikataba na hundi ya vikundi 2o vya wanawake wajasiriamali. 
 Wakazi wa Tarakea wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya polisi Tarakea.
Pichani kushoto ni aliyekuwa Katibu Mwenezi na Katibu wa Mbunge wa CHADEMA,wilaya ya Rombo John Tarimo akitangaza rasmi kurejea chama cha CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimsikiliza.
 Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wakirejesha kadi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo.

PICHA NA MICHUZI JR-ROMBO KILIMANJARO

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...