Dar es Salaam, Jumanne, Machi 3, 2015 – Serikali ya Tanzania itatoa taarifa ya Utekelezaji wa
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa! (BRN), Alhamisi; tarehe 5 Machi 2015, kuhusu
utekelezaji wa mikakati iliyowekwa katika Sekta Sita za Kipaumbele (NKRAs) zilizotekelezwa
katika mwaka 2013/14. Sekta hizo ni: Kilimo, Elimu, Nishati, Uchukuzi, Maji, na Utafutaji
Raslimali Fedha.
Ripoti ya Mwaka ya BRN imeandaliwa kuendana na utamaduni wa BRN wa kuweka
vipaumbele, malengo na mfumo wa utekelezaji unaoendana na uwekaji wa mikakati ya kina ya
kusimamia ufuatiliaji; pamoja na utumishi makini wa wafanyakazi wanaosimamia na kutekeleza
kwa uwazi.
Umma unaalikwa katika maonesho ya miradi ya BRN yatakayofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa Mlimani City kuanzia saa saba mchna hadi saa 11 jioni ili kupata fursa ya
kuufahamu zaidi mfumo huu na mikakati inayoendelea kutekelezwa.
Katika tukio hilo wananchi
pia watapata fursa ya kukutana na watekelezaji pamoja na walengwa wa miradi ya BRN, ambao
watazungumzia uzoefu wao kuhusu safari ya mabadiliko wanayoiona na jinsi mabadiliko ya
kiutendaji yaliyoletwa na BRN yanavyoboresha maisha yao.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...