Na Geofrey Tengeneza - Berlin 
Maonesho ya Utalii ya kimataifa ya ITB ya siku tano yameanza leo jijini Berlin. Maonesho haya yanayofanyika kila mwaka na ambayo ni makubwa kuliko yote duniani yanahudhuriwa na waoneshajio zaidi ya 10000 kutoka nchi 190 duniani. Tanzania katika maonesho haya inawakilishwa na waoneshaji 160 kutoka katika makampuni 60 kutoka sekta ya umma na binafsi . 
Taasisi za serikali zinazoshiriki maonesho haya ni Idara ya Utalii ya Wizara ya Maliaslili na Utalii, Bodi ya utalii Tanzania (TTB) ambao ndio waratibu wa ushiriki wa Tanzania katika maonesho haya. 
Nyingine ni Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mamlaka ya hifadhi ya ya Bonde la Ngorongoro (NCAA), Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na Jumuia ya Afrika Mashariki. 
Kwa mujibu wa Geofrey Meena Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania idadi ya makampuni na taaisi yanayoshiriki kutoka Tanzania katika onesho la ITB imekuwa ikiongezeka kila mwaka ambapo mwaka huu washiriki ni sitini (60) wakati mwaka jana jumla ya makampuni yalikuwa hamsini na tatu (53). Miongoni mwa matukio muhimu yanayotarajiwa ni pamoja na tukio la siku ya Jumuia ya Afrika Mashariki katika maonesho haya litakayofanyika tarehe 6/2/2015 ambapo Tanzania kama mwenyekiti wa jumuia hiyo itakuwa mwenyeji wa tukio hilo litafanyika katika banda la Tanzania. 
Mawaziri wa Utalii kutoka nchi wanachama, mabalozi wa nchi hizo hapa Ujerumani na wageni wengine mbalimbali waalikwa wanatarajiwa kujumuika na mwenyeji wao Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu katika hafla hiyo katika banda la Tanzania.
  Waoneshaji kutoka Tanzania wakiwa katika mazungumzo ya Kibiashara na wenzao kutoka nchi mbalimbali katika sikuu ya kwanza ya maonesho ya ITB jijini Berlin Ujerumani.
Waoneshaji kutoka taasisi za umma wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mweneshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi (wa tatu kulia) na Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena (wa Kwanza kulia) wakiwa katika kaunta ya banda la Tanzania katika maonesho ya ITB Ujerumani.
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mh. Philip Marmo (wa nne toka kulia)  katika picha ya pamoja na mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi za jumuia ya Afrika Mashariki nchini Ujerumani sambamba na maafisa kutoka Bodi ya Utalii Tanzania na Jumuia ya Afrika Mashariki muda mfupi baada ya kumaliza kikao cha pamoja kujadili imaandalizi ya ‘siku ya jumuia ya Afrika Mashariki’ katika maonesho ya ITB itakayo fanyika tarehe 6/2/2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...