Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema kujenga uadilifu kwa kila mtu katika nchi yake, ni kukataa rushwa kwa kutoa au kupokea.

Sefue aliyasema hayo katika Warsha ya Wadau ya kujadili Rasimu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi,Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi iliyoandaliwa na Tume ya Maadili iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam,alisema wazo la ahadi ya Uadilifu kwa viongozi,watumishi wa Umma na sekta binafsi ni mwanzo wa kampeni kwa nchi nzima.

Alisema sheria kali na adhabu,lakini iwe ni dhamira ya kila mmoja kufuata maadili na kujenga utamaduni wa kutotoa rushwa au kupokea rushwa.

Sefue alisema ahadi hizo zitatumika kama muongozo kwa kuzingatia makampuni yaliyotia saini pamoja na viongozi na watumishi wa umma katika utekelezaji wa majukumu yao, hivyo kutachangia  katika juhudi za kupambana  na rushwa nchini.

Aidha alisema lengo la 3.2 la dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025 inayohusu Uongozi bora na utawala wa sheria  inakusudia Tanzania kuwa jamii yenye maadili mema ,kuthamini ,utamaduni ,uadilifu,kuheshimu utawala wa sheria na kutokuwepo kwa rushwa na maovu.

Kwa upande wake Kamishina wa Tume ya Maadili, Jaji Mstaafu,Salome Kaganda, alisema rasimu ya ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi,Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi ni juhudi za kuunga mkono zilizopo za kukuza uadilifu uwazi na uwajibikaji katika kuimarisha utawala bora nchini.

Salome alisema kuwa walikuwa wakiangaliwa ni watumishi wa umma sasa watahusika sekta binafsi,wanasiasa na wafanyabiashara katika kujenga utawala bora katika nchi.

Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baara ya kufungua Warsha ya Wadau ya kujadili Rasimu ya Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi,Watumishi wa Umma na Sekta Binafsi iliyoandaliwa na Tume ya Maadili  leo katika ukumbi wa Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam
 Baadhi ya washikadau walioshiriki kwenye Warsha hiyo.
Picha ya pamoja.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...