Na Bashir Yakub.
Kipindi cha nyuma wakati nikieleza masuala ya sheria za ndoa niliwahi
kueleza utaratibu wa mgawanyo wa mali iwapo ndoa inavunjika. Kimsingi
nilieleza mgawanyo wa mali katika msingi wa uwepo wa ndoa ya mke
mmoja. Sikuwahi kueleza mgawanyo wa mali iwapo ndoa ni ya mke zaidi
ya mmoja. Wengi waliuliza swali hili ambapo baadhi niliwajibu na baadhi
sikuwajibu. Leo sasa nitaeleza mgawanyo wa mali katika ndoa ya mke zaidi
ya mmoja pale ambapo mmoja wa wake inatalakiwa .
1.NDOA YA MKE ZAIDI YA MMOJA.
Kwa jina la kitaalam ndoa za namna hii huitwa ndoa za mitala. Waolewaji
waweza kuwa wawili, watatu , wanne, watano au zaidi neno mitala hubaki
kuwa mitala. Sheria yetu ya ndoa inatambua ndoa ya mke zaidi ya mmoja
na hivyo kwa waliofanya hivyo hawajatenda dhambi yoyote kisheria. Ndoa
za namna hii mara nyingi zimekuwa zikifungwa na waislamu au watu
ambao huishi maisha ya kufuata mila ambao wengi wao wako vijijini. Hata
hivyo tumeshuhudia mazingira ya ndoa za namna hii kwa watu ambao ni
wa makundi tofauti na niliyotaja kwa siku za hivi karibuni. Yote kwa yote
hizo ndio ndoa za mitala.
2.ISEMAVYO SHERIA YA NDOA KUHUSU MKE ZAIDI YA MMOJA.
Kifungu cha 57 cha sheria ya ndoa kinaweka wazi kwa kusema kuwa, katika
sheria yoyote ile mwanaume anapokuwa na wanawake wawili au zaidi
wanawake hao wanatakiwa kuwa na haki sawa mbele ya macho ya sheria
na si vinginevyo. Kawaida tumezoea kuna u bi mkubwa na u bi mdogo. Basi
ieleweke kuwa hayo ni mambo ya kwetu lakini sheria haina u bi mkubwa
wala u bi mdogo. Sheria inajua mke ni mke awe alianza kuolewa au
ameolewa mwishoni. Wake wote wana haki sawa mbele ya mme wao na
mbele ya sheria na huo ndio msimamo wa sheria.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...